ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 13, 2015

WATANZANIA HOUSTON MNAKARIBISHWA KUREKODI NA KUZUNGUMZIA MAUWAJI YA ALBINO TANZANIA


Wadau kutoka New York wakirekodi kipindi kimoja wapo.

Wadau wa North Carolina wakiwa kwenye kipindi wakirekodi.

Timu ya Vijimambo ikishiriana na Kwanza Production inapenda kwanza kutoa pongezi kwa Watanzania Houston kwa jitihada zao za kupambana na mauawaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na pia ingependa kuandaa kipindi cha video ya kuongelea hili swala kwa mapana zaidi na kuangalia jinsi gani ya kukomesha mauaji haya ambayo yanaleta fedheza na aibu  ikiwemo ukiukaji wa haki za binadamu.

Kipindi kitarekodiwa siku ya Jumampili saa 8 mchana (2pm) mahali ni Extended Stay America chumba namba 224 anuani ni 2424 West Sam Houston Prkway, Houston, TX 77042. 

Kwa maelezo zaidi wasiana na 301 335 6383 asante

Ujumbe kutoka kwa ndugu zetu hapo chini.

2 comments:

Anonymous said...

mie wala sihitaji mazungumzo mareefu. siku nikishuka huko wanakowaua(Geita, Shinyanga, Sumbawanga etc) nitashuka na bastola yangu mkono mmoja na panga mkono mwingine, fyeka fyeka hao suspects wote, nikionyeshwa tu huyu ni suspect na-shoot.

mazungumzo tu bila vitendo hatuwezi kufika kokote, wataendelea kukatwa na kuuliwa unless operation kata kata inafanyika!

Anonymous said...

siku za uchaguzi zinakaribia tutaona sarakasi nyingi sana zikiletwa na magamba.

issue hii si ilikuwepo miaka ya nyumba sasa inajirudia tena na subirini uchaguzi ukiisha na magamba wakipata issue hii itakwisha.halafu msubiri siku ya uchaguzi ikitokea tena itafufulliwa.

hii ni kiini macho.