Waganda wanatumia kondomu bandia “buveera- zinazotenezwa kwa mifuko ya plastiki kutokana na uhaba wa Kondomu
Mahitaji yanafanya waganda kuwa wabunifu hata katika masuala ya kondomu.
Katika eneo la Kiyindi, wilaya ya Buikwe-mashariki ya Kampala, watu wanatumia kondomu bandia –wao huita “buveera- kutokana na mifuko ya plastiki.
Wenyeji wa Kiyindi wanadai ama kondomu ni ghali au hakuna kabisa.
Siraj Kalyango alifika huko kujionea kwa macho yake na aliporejea Kampala ametutumia taarifa ifuatayo.
Uganda inahitaji mipira ya kondomu million 20 kila mwezi hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya na tume ya Ukimwi takwimu za mwaka 2013.
Hata hivyo kondomu hizo hazitoshi na mahali zipo bei yake ni ghali mno haswa kwa taifa ambayo asilimia kubwa ya watu wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku.
''Hapa kwetu kweli kuna ukosefu mkubwa sana wa mipira ya kondomu ,imezidi matarajio ya wengi na hivyo inawalazimu watu kustarehe mwili kwa mwili na unajua tena hiyo ni hatari sana maanake
waweza kuambukizwa magonjwa mengi na tena yale ambayo hayana tiba''anasema mkaazi wa kiyingi.
''Wakati mwengine ukiwa nayo unaitumia lakini je ukikosa ?''Mifuko ya plastiki inatumika kwa wingi miongoni mwa jamii ya wavuvi
Hawa ni baadhi tu ya wenyeji wa mji wa Kiyindi iliyoko karibu na ufukwe wa ziwa Victoria katika wilaya ya Buyukwe nchini Uganda.
Mwanasosholojia , Derick Motema ambae alikwenda Kiyingi miezi michache iliiambia BBC yaliyomfika.
''Mwanamke mmoja alinivuta na kuiniingiza ndani ya chumba chake akataka kufanya kitendo cha ngono kwa malipo, nikamuuliza iwapo anamipira ya Kondomu akasema hana lakini akasema kuwa
alikuwa na karatasi za plastiki ambayo tungeifunga kwa mipira ya elastiki (bladder) alisema Motema
''Tulikuja hapa Kihindi miezi miwili iliyopita kuhudhuria kongamano la kimatibabu iliyoandaliwa na mbunge wa eneo hili .
Nilikuwa naongoza kundi ambalo lilikuwa linanyunyuzia dawa ya kuuwa wadudu kama vile kunguni ndani mwa nyumba za wakazi huko.
Katika pitapita yangu nikafika kwenye danguro ambako kulikuwa na makahaba wengi.
Waliponiona wakanijia wakidhani kuwa mie ni mteja na mmoja wao akanivuta hadi ndani ya chumba chake.
Ndani huko akaniomba hela ili tufanye kitendo cha ngono.Uhaba wa Kondomu unatokana ukosefu wa wahisani
Mie nikamwambia kuwa sikuja kufanya hilo ,lakini yeye akang'ang'ania kufunga lango.
Sasa nikawambia ikiwa anataka tufanye kitendo hicho nikataka kujua ikiwa walikuwa na mipira ya kondomu na nilitaka kuinona.
Akaniambia hana mipra ya kondomu lakini akapendekeza kuwa wanakondomu mbadala ya mpira wa plastiki naweza kuivaa na nikaifunga mipira ya raba.
Mambo hayo yalinigusa sana kwani nilifikir kuwa kuna baadhi ya wanaume ambao wanatumia hizo kondomu mbadala.
''Ukweli ni kwamba wanawake makahaba wapo hapa chungu nzima anasema mkahazi mwengine wa eneo hilo Omari Ejaga.
Kiyindi ni kituo cha biashara ambacho kinapatikana kandokando mwa Ziwa Victoria katika wilaya ya Buikwe umbali wa kilomit 120- mashariki mwa jiji kuu la Kampala.
Kina watu wengi kutoka sehemu tofauti za nchi pamoja na je yake ambao wengi wanajihusisha na uvuvi il hali wengine na biashara mbalimbali.
Nilifika mahali pa danguro alilotaja Bw Motema kutaka kujua ukweli ikwa wanatumia mifuko ya plastiki badala ya kondomu, lakini juhudi zangu ziliambila patupu akina mama hao walipogundua kuwa mimi ni mwandishi habari .
Bi Annet Nabasinda ni mfanya biashara ya kuuza vifaa vya kuwarembesha wanawake .Wanaume wengi hawataki kutumia mipira ya Kondomu wakidai inawapunguzia hisia
Nilimuuliza mtazamo wake iwapo matumizi ya mipira ya kondomu ni makubwa Kiyingi ,lakini akakanusha .
Annet anasema kuwa katika mtaa huo si ajabu kumuona mwanamke ambaye anajulikana wazi kuwa ni mgonjwa lakini wampata ana mimba.
Mfanyakazi wa kituo cha afya cha jamii Makonge –Kiyindi Justin asema kuwa kiwango cha kuenea kwa UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa katika wilaya ya Buikwe ni kubwa mno.
Anasema kuwa kondomu hazitoshi kwa sababu yamkini wahisani wamepunguza usambazaji wake kufuatia mtafarauku na serikali kufuatia kupitishwa kwa sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Aidha anasema kuwa japo watu wana hela lakini hawataki kununulia mipira ya kondomu bali huamua kununua vitu vingine vya dharura kama vile chakula na mahitaji mengine ya kila siku.
Buikwe inakuwa ya nne kwa idadi ya maambukizi kwa kuwa jamii kubwa inajihusisha na biashara ya samaki usambazaji ni mkubwa.
''Sina takwimu ninazoweza kulinganisha lakini kasi ni kubwa kuliko ya taifa ya 7.5 au 7.6 anasema.
''Kwa hivyo ikiwa kuna msamaria mwema anaeweza kuleta kondomu na kuzigawa kwa jamii litakuwa jambo jema kwani kuna mahakaba wengi hapa'
lakini tunamshukuru Mungu kuwa wako hiari kupimwa Ukimwi ukiwafikia''.Wanawake wa jamii hiyo wanadai hawawezi kuishi bila ya ngono japo waume wao wamekwisha aaga kutokana na ukimwi
Hata hivyo afisa wa chama cha msalaba mwekundu Kiyindi yeye anasema akuwa kondomu zipo za kutosha ila watu ndio hawataki kuzichukuwa.
Ameongeza kuwa wengine wanaona haya kuuliza kondomu madukani na hata katika zahanati za afya.
Kauli yake inapingwa na baadhi wakitoa sababu ambazo Bi Anne Nabasinda amezisikia.
''Wanaume wengi wanasikika wakiwauliza hawa machangudoa iwapo wamewataka hao inakuwaje wanawataka watumie mipira ya Kondomu ama plastiki''
''Wengine wanadai kuwa wazungu wameweka vitusi vya ukimwi katika mipira ya kondomu iliwapunguze idadi ya Afrika'' anasema Annet Nabasinda .
Ama kweli mahitaji yanamlazimisha mwanadamu kujikuna kichwa lakini hatua wakazi wa Kiyindi Biukwe kutumia 'karatasi za plastiki za mkate -buveera'' kama kondomu mbadala si jambo la kuigwa.
No comments:
Post a Comment