ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 12, 2015

Mwansasu: Tupo tayari dhidi ya Misri



Kocha akiwa na wachezaji wa soka la Ufukweni

John Mwansasu amesema anatarajia ushindi dhidi ya Misri siku ya Ijumaa wakati timu hizo zitakapopambana katika michuano ya kufuzu ya kucheza Fainali za Afrika za soka la ufukweni zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli mwezi Aprili mwaka huu.
Mchezo kati ya Tanzania na Misri utafanyika Ijumaa majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es salaam.

Mwansasu, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania amesema wapo vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.

Timu ya Misri imewasili Dar es Salaam siku ya Jumatano na wanaendelea na mazoezi katika uwanja utakaochezwa mechi hiyo ili waweze kuozea.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo, ambapo kwa takribani wiki mbili kipo kambini Bamba Beach wakijifua kwa mchezo huo.

Tanzania ilifuzu hatua ya pili baada ya kuiondoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12 -9, na endapo itafanikiwa kuwaota Misri, itafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za soka la Ufukweni zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli mwezi April mwaka huu.

Waamuzi wa mchezo huo ni Eid Haitham Eid Hassan (Sudan), mwamuzi msaidzi wa kwanza Abaker Mohamed Bilal (Sudan), mwamuzi msaidizi wa pili Abdalla Hassain Hassaballa, mtunza muda (time-keeper) Boubaker Bessem (Tunisia) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Khiba Herbert Mohoanyane kutoka Lesotho.

No comments: