Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akizungumza (alhamisi) katika majadiliano ya jumla katikamkutano wa Kamisheni 59 kuhusu Hadhi ya Wanawake. Mhe. Waziri anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwamo wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Tanzania ni kati ya nchi 13 zinazoiwakilisha Afrika katika Kamisheni hii inayoundwa na nchi 45.
Katika picha hii ya maktaba anaoneka Mhe. Asha-Rose Migiro ( Mb) wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na baadhi ya askari wanawake kutoka JWTZ wanaoshiriki katika operesheni ya kulinda amani kupitia Umoja wa Mataifa huko Lebanon. Katika mchango wake, Mhe. Simba pamoja na mafanikio mengine ambayo Tanzania imeyapata katika miaka 20 tangu mkutano wa Beijing ni pamoja na askari wanawake kupata fursa za kushiriki katika operesheni za kulinza amani zinazoratibiwa na Umoja wa Mataifa.
Pamoja na kuzungumza katika majadiliano ya jumla, Mhe Waziri Sophia Simba pia alipata fursa ya kuhushiriki Mkutano wa Mawaziri kutoka Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afrika karibu na UN. Mkutano huo ulikuwa wa kujadiliana na kupitisha maazimio mbalimbali kuhusu maudhui ya mwongo wa wanawake wa Afrika. Pichani Mhe. Waziri akiwa na Katibu Mkuu wake Bi. Anna Maembe wakifuatilia majadililano hayo
Sehemu ya ujumbe wa Mawaziri kutoka nchi za Afrika wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nchi za Afrika
Na Mwandishi Maalum, New
York
Ushiriki wa askari wanawake katika
Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja
wa Mataifa, ni baadhi ya mafanikio ambayo Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inajivunia miaka 20 baada ya Mkutano wa Kihistoria wa wanawake
uliofanyika Beijing, China mwaka 1995
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb) ameyasema
hayo leo ( alhamis) wakati alipokuwa
akitoa tathmini na changamoto za utekelezaji wa
maazimio muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo wa wanawake Beijing.
Mhe. Waziri Simba, anaongoza ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Hadhi ya Wanawake ( CSW)
unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa, katika Ujumbe huo wa Tanzania unajumuisha na washiriki
kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
akiwamo Mhe. Zainab Omar Mohammed, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii,
vijana, wanawake na watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“ Katika miaka miaka
20 iliyopita, yapo mambo mengi
ambayo Tanzania tumepiga hatua za kuridhisha, katika maeneo ya uwezeshwaji na fursa sawa kwa wanawake. Katiba za pande
zote mbili za Muungano zinaainisha vema
kuhusu hadhi ya mwanamke. Na
Katika katiba mpya inayopendekezwa
hivi sasa kuna eneo
ambalo linazungumzia kwa kina Usawa wa Jinsia na Uwezeshwaji wa
wanawake.” anasema Waziri Simba
Vile vile ameeleza baadhi ya sheria ambazo ama zimefanyiwa marejeo au kutungwa kwa
lengo la kuboresha usawa wa kijinsia. Amezitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni sheria zinazohusu watoto, sheria zinazohusu usafirishaji wa
binadamu, sheria ya ardhi, HIV/AIDS na
sheria ya makosa ya kujamiana.
Kuanzishwa kwa dawati la jinsia na watoto
katika vituo vya Polisi, vituo vya kuhifadhi watoto,
vituo kwaajili ya wanawake
wanaofanyiwa ukatili na mtandao wa viongozi wa madhehebu ya dini kuhusu ukatili
dhidi ya wanawake. Ni baadhi ya mafanikio ambayo yameelezewa na Mhe. Waziri
Ameeleza zaidi kwa kusema, Wanawake wengi sasa wanashiriki
katika siasa ambapo kwa mfano asilimia 36 ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ni
wanawake na kwa upande wa Zanzibar
asilimia 33 ya Wawakilishi ni wanawake.
Na kwamba kumekuwapo
pia ongezeko la idadi ya wanawake Majaji na Mahakimu na wanaoshika nafasi
za uongozi.
Mhe. Simba amewaeleza wajumbe
wanaoshiriki mkutano huo kwamba katika kuhakikisha panakuwa na fursa sawa katika ajira utumishi wa Umma, kuna
kifungu katika sheria za
utumishi wa umma vinavyoainisha kwamba
pale mwanamke na mwanaume
wanapokuwa na sifa zinazolingana, basi mwanamke atafikiriwa kwanza.
Kwa upande wa elimu, pamoja na
kuwa na uwiano sawa kati ya
wavulana na wasichana katika shule za msingi. Anasema elimu ya msingi inatolewa bure katika shule za serikali
na kwamba utaratibu huo pia utafanyika
katika shule za sekondari
za umma. Aidha ameelezea ongezeko
la wanafunzi wa kike wanaochukua masomo ya sayansi.
Kwa upande wa Afya, Mhe. Waziri amesema Tanzania imepiga hatua za kuridhidha katika
upunguzaji wa vifo vya wanawake
wajawazitio na vya watoto wachanga.
Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo na mengine mengi ambayo Tanzania inajivunia kuhusu hadhi ya wanawake
na watoto wa kike, anasema kama ilivyo
kwa mataifa mengi yanayoendelea, Tanzania pia bado inakabiliwa na changamoto
nyingi zikiwamo za uhaba wa fedha kwa
miradi inayohusu masuala ya jinsia, ndoa na mimba za utotoni, umaskini wa kaya na ukatili dhidi ya
wanawake.
Mhe. Waziri Simba, Tanzania
imejifunza kutokana na changamoto hizo na nyinginezo na kwamba imejipanga vema
kutekeleza baadhi ya changamoto
hizo hususani upunguzaji wa umaskini, kupitia malengo mapya ya maendeleo endelevu
baada ya 2015.
No comments:
Post a Comment