Advertisements

Wednesday, March 4, 2015

Waziri Membe azungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataiafa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) waliopo hapa nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. Masuala hayo ni pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na mauaji ya Albino, Mkataba wa Makubaliano ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini na Hali katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kama DRC. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tarehe 03 Machi, 2015 
Sehemu ya Mabalozi na Wajumbe wengine waliohudhuria mkutano kati yao na Waziri Membe (hayupo pichani) wakifuatilia mazungumzo. Mwenye tai nyekundu ni Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Mark Childress. 
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wawakilishi. 
Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Mabalozi. 
Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Sinikka Antila akichangia jambo wakati wa mkutano kati ya Mabalozi na Mhe. Waziri Membe. 
Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Chirau Mwakwere akifuatilia mkutano kati yao na Waziri Membe. 
Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (kushoto) akiwa na Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing pamoja na Balozi wa Uingereza, Mhe. Diana Melrose. 
Mabalozi wakati wa mkutano 
Mkutano ukiendelea huku Mabalozi wakifuatilia 
Mmoja wa Mabalozi akichangia hoja wakati wa mkutano 
Mkutano ukiendelea 
Picha ya Pamoja Picha na Reginald Philip

No comments: