Advertisements

Tuesday, April 14, 2015

Buhari:Tutawarejesha wasichana wa Chibok




Maelfu wamejitokeza kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutekwa kwa wasichana hao wa Chibok

Huku Nigeria na ulimwengu kwa jumla ukiadhimisha mwaka mmoja tangu kutekwanyara kwa zaidi ya wanafunzi wasichana 200 na wapiganaji wa Boko Haram

rais mteule jenerali mstaafu Muhammadu Buhari amesema kuwa atafanya kila awezalo ili kuwarejesha nyumbani wasichana hao.

Lakini Buhari amekiri kuwa baadhi ya wasichana hao huenda wasipatikane tena.Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari amesema kuwa atafanya kila awezalo ili kuwarejesha nyumbani

Siku ya Jumatatu,mkaazi mmoja wa mji wa Kazkazini Mashariki wa Gwoza amesema kuwa aliwaona baadhi ya wasichana hao

wiki tatu zilizopita walipokuwa wakitoka ndani ya nyumba kubwa karibu na kwake.

Maadhimisho ya kutekwa nyara kwa wasichana hao kutoka shule moja ya Chibok yanafanywa kupitia mikusanyiko na maandamano nchini Nigeria pamoja na duniani kwa jumla.

Ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za kibinadamu Amnesty International inasema kuwa takriban wanawake 2000 na wasichana wametekwanyara na Boko Haram tangu mwanzo wa mwaka uliopita.Ni mwaka mmoja tangu kutekwanyara kwa zaidi ya wanafunzi wasichana 200 na wapiganaji wa Boko Haram

Awali rais anayeondoka mamlakani nchini Nigeria Goodluck Jonathan, alisema amesikitishwa kuwa siasa zilipewa kipau mbele,

kuliko maslahi ya wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram kutoka shule moja kwenye mjiwa Chibok katika jimbo la Borno.

Rais Jonathan, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wiki mbili zilizopita anasema kuwa bado ana uhakika kuwa wasichana hao waliotekwa nyara mwaka mmoja uliopita watapatikana wakiwa salamaWasichana wa shule waliotekwa nyara na Boko Haram

Msemaji wa kundi linalojiita Bring Back Our Girls ,Aisha Yesufu, aliiambia BBC kuwa serikali ya rais Jonathan kwanza haikuamini kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa.

Lakini rais Jonathan alikilaumu chama cha upinzai kinachosimamia jimbo na Borno kwa kusababisha mchanganyiko wakati wasichana hao walipotekwa.

No comments: