ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 22, 2015

DIABY WA ARSENAL KUCHEZA KWA DEIWAKA


Diaby kupiga ‘deiwaka’ Arsenal?


Kiungo wa Arsenal, Abou Diaby anamaliza mkataba wake Emirates akiwa amecheza mechi 16 tu katika misimu minne, lakini The Gunners wanaona ugumu kumuacha aondoke.
Ameshindwa kucheza kwa sababu ya majeraha ya kila mara, hivyo kwamba amekuwa akilipwa mshahara bila kufanya kazi na sasa ‘Profesa’ Arsene Wenger anafikiria kuandika mkataba mpya, ambapo Mfaransa huyu atalipwa kwa kadiri atakavyocheza.
Wenger ni mtu mwenye heshima kubwa kwa mchezaji wa kaliba ya Diaby na amekuwa wakati wote akitafuta jinsi ya kumrejesha kwenye kikosi cha kwanza. Amepona majeraha yake na majuzi alicheza na kikosi cha U-20 sambamba na Mikel Arteta na Mathieu Debuchy.
Kadhalika inaelezwa kwamba Wenger yu tayari kuona Diaby (28) akiendelea kupewa huduma na Washika Bunduki wa London hadi arejee hali ya kawaida hata kama hakutakuwapo mkataba rasmi, ili baada ya muda afanyiwe tathmini juu ya utimamu wa mwili wake.
Ni katika hali hiyo, Wenger amependekeza kwamba ikiwa Diaby atakubali basi alipwe kwa kadiri ya mechi atakazokuwa akicheza, kwa sababu haieleweki ni lini na wapi ataumia.
Imekuwa kawaida akirejea uwanjani hakosi kuondoka na majeraha katika kipindi kifupi na humweka nje kwa muda mrefu. Licha ya kifundo cha mguu amepata kuugua goti
Matatizo yake yalitibuka baada ya kuvunjika kifundo cha mguu 2006 na tangu hapo amekuwa akiumia hapo au kiungo kingine. Wenger amekuwa akisema rafu ya beki waSunderland, Dan Smith ndicho chanzo cha matatizo ya Mfaransa mwenzake huyo anayelipwa pauni 65,000 kwa wiki.
“Diaby hana tatizo la akili bali la kuumia. Ni mchezaji ninayemheshimu sana. Kila akirudi uwanjani anaumia na kuanza tena kwenye sifuri, aliharibiwa na rafu mbaya inayomsumbua hadi sasa. Akirudi nitambakiza kundini, daima ninamwamini,” anasema Wenger. Mkataba wa Diaby aliyesajiliwa Januari 2006 unamalizika msimu wa kiangazi na Wengere anasema ameshazungumza naye, ni kiasi cha mwenyewe kufanya uamuzi kabla ya kukutana tena kuhitimisha mazungumzo.
Credit:TS

No comments: