ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 29, 2015

DKT. SHEIN MGENI RASMI UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI RUVUMA.


Na: Frank Shija, WHVUM


Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2015 ambazo Kitaifa zinafanyika Mkoani Ruvuma.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waizri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakati wa mazoezi ya ya mwisho yaliyofanyika katika Uwanja wa mpira wa Majimaji mjini Songea.

Waziri Fenella amesema kuwa maandalizi yameenda vizuri na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za uzinduzi wa mbuio za Mwenge na kutoa hamasa zaidi kwa Vijana wotye nchini kushuhudia uzinduzi huo ata kwa vile utaonyeshwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).
"Nisema tu kuwa maandalizi yamekwenda vizuri sana mmejionea vijana wa Halaiki walivyo onyesha umahiri wao, niwatate tu wakazi wa mjini wa Songea mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia sherehe hizi za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru lakini pia VIjana nchini kote shuhudieni tukio hili muhumu kwa kuwa litaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC" Alisema Dkt.Fenella
Aidha Waziri Fenella alitoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika zoezi a kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura na baadaye watumie demokrasia kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2015 zinazindulia rasmi tarehe 29 Aprili 2015 mkoani Ruvuma na kilele chake kitakuwa tarehe 14 Oktoba mkoani Dodoma ambapo mbo hizo kwa mwaka huu zimebeba kauli mbiu ya "Tumia Haki yako ya Kidemokrasia" Jiandikishe na kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 

Mwenge huo wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri 168 za mikoa 30 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments: