Advertisements

Saturday, April 4, 2015

JK ateuliwa Mwenyekiti jopo la majanga ya afya duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemteua Rais Jakaya Kikwete kuwa Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya (High - Level Panel on Global Responses to Health Crises).

"Ni majukumu makubwa na yenye changamoto nyingi lakini dunia inahitaji tuwe na mikakati katika masuala haya ambayo ni muhimu kwa maisha ya binadamu, hivyo hatuna budi kufanya kazi hii kama mchango wetu kwa ajili ya maisha ya wanadamu na dunia kwa ujumla," alisema Rais Kikwete mara baada ya uteuzi huo.

Wengine walioteuliwa katika jopo hilo ni Delos Luiz Nunes Amorim wa Brazil, Micheline Calmy-Rey wa Switzerland, Marty Natalegawa wa Indonesia, Joy Phumaphi wa Botswana na Rajiv Shah wa Marekani.

Jopo hilo linatarajiwa kufanya kikao chake cha kwanza mapema Mei, mwaka huu na linatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu mwishoni mwa Disemba, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:

Anonymous said...

Asante kwa kumpatia nafasi hiyo muhimu na tunamwomba aanze na nyumbani kwake ambako ndiko kuliko na matatizo hayo saaana.