ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 14, 2015

KENYA WAFA KIUME WAPIGWA 6-1 NA FC KILIMANJARO NCHINI SWEDEN

Timu ya Tanzania, FC Kilimanjaro ambayo ni mabingwa wa soka la Afrika nchini Sweden imepata ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya watani wao wa jadi Kenya kwenye mechi maalum ya kirafiki ya Amani na Upendo iliyofanyika jijini Stockholm jana tarehe 11 Aprili, 2015

Mechi hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Balozi za Kenya na Tanzania nchini Sweden kwa kushirikiana na wanadiaspora wa nchi hizo kwa madhumuni ya kuonyesha mshikamano na kuziombea nchi zetu amani na upendo kufuatia matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni nchini Kenya. 
Baadhi ya wachezaji wa FC Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja.
Benchi la timu ya FC Kilimanjaro.
Mpambano ukiendelea.
Masahbiki wa FC Kilimanjaro wakifuatilia mpambano
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments: