Rais wa TFF, Jamal Malinzi.Moja ya mechi ambazo zimepanguliwa ni kati ya Simba dhidi ya Mgambo Shooting ya Tanga ambayo awali ilitarajiwa kuchezwa Jumapili Aprili 12 lakini sasa itapigwa Aprili 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi nyingine iliyopanguliwa kutokana na maveterani hao ambao awali walitarajia kuchuana na nyota wa zamani wa timu ya Tanzania (Taifa Stars) Machi 28, mwaka huu ni kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City ambao umesogezwa kwa siku moja.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema mabadiliko hayo yanachangiwa na wamiliki wa Uwanja ambao ni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoa ruhusa kwa shughuli nyingine kutumika kwenye uwanja huo.
Kizuguto alisema baada ya Bodi ya Ligi na Kamati ya Mashindano kupanga ratiba, wanaipeleka wizarani na hapo mambo yanakwenda kama yalivyotarajiwa endapo uwanja huo wa Taifa hautakuwa na shughuli nyingine zilizopewa kibali cha kutumika.
"Ila mabadiliko ya sasa yameiangalia na Yanga ambayo bado inashiriki mashindano ya kimataifa, ndiyo maana sasa itacheza Jumapili badala ya Jumamosi, halafu Jumatano na mchezo wa Simba ukapelekwa mbele zaidi," alisema Kizuguto.
Mechi nyingine iliyoonekana kutokuwapo katika ratiba ni ya leo kati ya Yanga na Coastal Union kutoka Tanga ambapo wageni hao hawakuwa wakiifahamu hapo kabla, mpaka juzi mchana walipopata taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wa Bodi ya Ligi.
Hivi karibuni Rais wa TFF, Jamal Malinzi, alikaririwa akisema mabadiliko ya mara kwa mara ya ratiba ya ligi yamewashushia heshima na kuahidi tukio hilo kutojirudia tena katika msimu ujao.
Kabla ya mechi mbili za ligi kuchezwa leo, Azam ndiyo timu inayoonekana imecheza mechi chache 18, wakati nyingine zimeshashuka dimbani mara 21.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment