ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 8, 2015

MPANGILIO WA CHACHANDU HUONGEZA LADHA YA CHAKULA

Aka babu acha nicheke miye, Mungu kanipa uzima na afya tena yenye furaha mdomoni meno ya sebuleni yapo, katikati mwanya wa uchokozi pembeni kidogo jino la dhahabu kwa nini nisicheke kuonesha nilichonacho.

Najua mwenye mapengo anaona kama sikumtendea haki, jamani kucheka si lazima uwe na meno hata ukiwa huna meno we cheka tu tena jiachie mate yakiruka waombe msamaha kwani raha ya kucheka ufurahishwe.
Basi ngoja nikupashe kuhusiana na mada ya wiki iliyopita kuhusu kina baba kutugeuza dada zao, nusura ivunje nyumba ya kigogo fulani jina kapuni ila ukitaka nitafute kwa wakati wako.

Kumbe tabia yake kila akirudi kwa mkewe hujifanya amelewa na kushindwa kumpa haki yake iliyomtoa kwa baba na mama yake ambayo huipati kwingine bali kwa mtu aliye haramu wako. Japo siku hizi dunia imevaa suti kina baba wanakula mayai yao wengine wanasema mtoto wa kike faida mama mtaji.

Kuna siku nilijua siri ya kina baba kutembea na watoto wao wa kike, amini kama huamini siyo lazima. Kina baba wengi wanaotembea na watoto wao wa kike hutokana na kuchukua mama shepu mbaya lakini mtoto akizaliwa mmmh, kweli fyatulio la ubao halitoi tofali la mbao bali la mchanganyiko wa sementi, mchanga na maji.
Basi mtoto akipita pengine Mungu kamjalia makalio ya utata, baba hummezea mate na kujikuta akiona watu wengine wanafaidi wakati mbegu katia mwenyewe.

Mmmmh mbayaaaaaa eeeeeh, haipendezi mwanao ni mwanao kama ungetaka wanawake wenye makalio makubwa kwa nini ulimuoa mwanamke aliyebeba sinia nyuma.Si kwamba nawadhalilisha wasio na makalio makubwa, la hasha naongea na wanaume waliokatika mishipa ya aibu na kutawaliwa na fikra za ngono. Ukweli unabakia palepale kila mtu ana matamanio yake wapo wanaopenda wenye maumbile ya kimisi kwa kuona kuwa hawachoshi haraka kuliko wanawake wanene wenye makalio makubwa kuwa hao ni wavivu kitandani hujitupa kama mzigo.

Hebu tuachane na hayo tuzungumzie kilichokufanya ushike gazeti na kutupia macho kwenye kona hii. Kuna kitu kimoja leo nataka nizungumze na wanawake wenzangu, kwanza napenda kusema hili wanawake tupunguze ulimbukeni kila kitokacho lazima ukifanye, aaaah siyo hivyo ndiyo maana wanatutoa akili.

Leo nazungumzia chachandu za kiunoni, kumekuwa na mtindo mpya wa kuunganisha chachandu tatu mpaka nne na kuwa moja ukiangalia utafikiri mwanamke amevaa mkanda, anakuwa nazo zaidi ya kumi na kupoteza ramani ya kiuno .

Basi nataka kuwaeleza leo kuvaa michachandu mingi bila mpangilio huwaboa wanaume. Raha ya chachandu ikae mojamoja hata kama utavaa kumi lakini zipishane ili mshikaji aweze kuzichezea mkononi kwa kuzihesabu hata wewe mwenyewe zinapokupapasa kwa kuzunguka kwenye uzi hukutia msisimko wa mahaba, siyo rundo la chachandu kama fundo la msuli.

Narudia siyo kila kitu lazima tukifanye ila ni muhimu kabla ya kukifanya umuulize mpenzi wako anavutiwa na mtindo gani wa chachandu kuliko kuyajaza kama mkanda wa jeshi.
Kwa haya machache tukutane wiki ijayo.

GPL

No comments: