Advertisements

Saturday, April 18, 2015

MTANANGE WA YANGA NA ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA UWANJA WA TAIFA


Goli la kwanza la Yanga katika DK ya 2 tu ya mchezo lilifungwa kwa njia ya penati baada ya Msuva kufanyiwa madhambi ndani ya 18. Na naodha wa Yanga Canavaro akakwamisha wavuni mpira huo kama unavyoona golikipa Etoile akipishana nao na kudaka upepo.


Mchezaji wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, Bounedjah Baghdad akiangalia namna ya kuwatoka wachezaji wa Yanga, Mbuyu Twite na Amissi Tambwe wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho unaoendelea kupigwa hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Kipindi cha pili kimeanza hivi punde na matokeo ni 1-1.Picha zote na Othman Michuzi.
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiruka daluga la Beki wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho unaoendelea kupigwa hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Kipindi cha pili kimeanza hivi punde na matokeo ni 1-1.
Wachezajiwa Timu ya Yanga, wakishangilia ushindi sambamba na mashabiki wao.
Kiungo wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, Franck Kom aruka juu kuwania mpira wa kichwa wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho unaoendelea kupigwa hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Kipindi cha pili kimeanza hivi punde na matokeo ni 1-1.
CREDIT:JIACHIE

1 comment:

Anonymous said...

kama kawaida yetu safari ya yanga itaishia hapa