Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb) akimpokea Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Mwalimu Nyerere kwa ajili ya semina hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb) akimpokea Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Mwalimu Nyerere kwa ajili ya semina hiyo.
Rais Mstaafu Mkapa akiteta jambo na Mhe. Membe wakati wa semina hiyo ambapo alizungumzia changamoto za ushirikiano wa kiuchumi na diplomasia nchini Tanzania, na nje ya nchi na Jumuiya za Kimataifa. Andiko la mada hii litapatikana baada ya muda mfupi kwenye tovuti ya Wizara.
Mabalozi, Maofisa na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Walimu na Wanachuo cha Diplomasia wakimsikiliza kwa makini Mhe. Benjamin W. Mkapa.
Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akitoa mada katika semina ya masuala ya diplomasia ya kiuchumi kwa Mabalozi, Maofisa na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani). Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 9 Aprili 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (mbele kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Balozi Irene Kasyanju wakifuatilia
Wajumbe wa semina wakimsikiliza kwa makini Balozi Mlay (Mstaafu) (mbele kushoto aliyesimama) akitoa maoni yake kuhusu mada iliyowasilishwa katika semina
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga akiuliza swali kufuatia mada iliyotolewa na Rais Mstaafu Mhe. Mkapa katika hiyo semina hiyo.
Picha ya pamoja Rais Mstaafu Benjamin W. Mkapa (katikati), Mhe. Bernard Membe na Balozi Rajab Gamaha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Maafisa Mambo ya Nje.
No comments:
Post a Comment