ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 23, 2015

TAARIFA KWA BLOGGERS KUHUSU UANDIKISHAJI WANACHAMA 'TANZANIA BLOGGERS NETWORK' (TBN)

Chama cha Wamiliki/ Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN   kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika 
 ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania  wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa  mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana  kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo  mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha  mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/-  ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa  kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN.

 Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia  saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN,  Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu  na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili. 

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama  watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa  kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa  muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga  uwanachama wa TBN. 

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani  yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda  za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha  mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida),  Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera,  Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na  Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa  muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika 
kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini copy, lakini copy hiyo wataigharamia  wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za  TBN. 

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470 
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)



1 comment:

Anonymous said...

Hamuwezi kiambia watu wajiunge, walipe ada na gharama zote bila ya kutoa maelezo ya nini faida ya uwanachama huo? Toaeni maelezo ya kutosha