ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 13, 2015

TANZANIA MPYA YACHANGIA $3000 KWA AJILI YA KUSAIDIA WALIO ZALIWA NA UALBINO

TANZANIA MPYA, kundi la whatsaap la watanzania wanadiaspora lilianzishwa kwa lengo la kuwaunganisha vijana kwa ajili ya kujishirisha katika mijadala ya mawazo ya kuleta chachu ya maendeleo katika jamii ya watanzania marekani na nyumbni Tanzania.

Kundi hili limewahusisha vijana wenye taaluma mbalimbali kwa lengo la kurejea matatizo ya jamii na taifa lao la Tanzania, na kuangalia wajibu na uezo wao katika kushiriki kupigana na changamoto hizo.

Vijana hawa wakidai kuwa wamechoshwa na hulka ya waliowengi, kukaa pembeni na kulaumu serikali.

Akidai Admin wa kundi hili Bwana Nassor Basalama kuwa kazi ya kujenga nchi ni ya wananchi. Sasa ikiwa mwananchi ndio anayefanya kazi ya kulalamika, nani atakaye fanya kazi ya kujenga? Hii ni hulka ya kukosa miono naya kifukara ya kutafuta kujiridhisha kwa kutobeba majukumu mazito ya ujenzi wa taifa.

Kundi hili limewahusisha viongozi wa Jumuiya zote za watanzania marekani, na taasisi mbalimbali.
Wiki 2 zilizopita kundi hili lilikabidhi $3000 kwa NGO ya Albino charity na AFROBINO kwa lengo la kusaidia watanzania wanaoathirika kwa ugonjwa wa ngozi na macho. Pia kundi hili limeandaa powerpoint ambayo imeisambaza kwa jumuiya za watanzania na kwa ajili ya kuelimisha juu ya Albinism.

2 comments:

Anonymous said...

Hii ni dhana nzuri sana ambayo inahitaji kupongezwa. Simanzi langu ni pale ninapobadilisha hizi dollar 3000 ambayo ni kama shilingi milioni tano ambazo hazitoshi hata kununua mboga kwa wale establishments. Ombi langu kwa watanzania especially walioko nje ni kuelewa kwamba tatizo letu watanzania sio fedha, rather ni elimu ya jamii itakayo jumuisha uwajibikaji. Kwa maendeleo yenu ya technologia, ingekuwa busara kama mngeanzisha uzambazaji rahisi wa elimu kuwaelewesha wananchi kwamba serikali ni mali yao na ipo hapo kwa matakwa yao na inatakiwa kuwafanyia kazi wao na sio other way around. Vinginevyo vijisenti vyenu havitasaidi chochote kwa nikiduchu zisizotosha hata kulipia bili ya simu ya mheshimiwa.

Anonymous said...

Bwana Anonymous, mimi Naitwa Nassor Basalama. Ni kweli kabisa inawezekana hii pesa Isitoshe hata kulipia simu (hususan ya watu wazito kama wewe). Unajua ndugu yangu sio hizi pesa hazitoshi hata kulipia nsimu, ni vitu vingi tu hazitoshi. napenda kuamini kuwa unadhana au dhamira safi, ili jibu langu liwe na manufaa kwako.
Unajua kitu chochote unachokiweka au peleka pasipo stahiki, huwa hakitoshi. Ngoja nikupe mfano; ukimchukua kijana msomi mzuri, mwenye upeo mkubwa. Ukampa kazi ya kila kukicha kukosoa serikali, kwa hakika utakuwa umefanza uzembe wa hali ya juu sana, na hilo litakuwa ni janga la taifa.

Unajua $3000 utakuwa umeondoa kadhia ya maumivu ya ngazi yanayo tokana na jua kwa watoto wangapi? Unajua $3000 utakuwa umesaidia watoto wangapi juu ya maumivu ya macho wanayoyapata kila siku ya Mungu?

Mimi ningekushauri ndugu yangu kwa nia safi. Kuwa mfano ili usikilizwe. Tena mimi nitakuwa wa mwanzo kukusikiliza "Bwana Anonymous".

Nashukuru kwa ushauri wako

wako N.Basalama