Advertisements

Wednesday, April 22, 2015

TUZO ZA RAIS KWA MAKAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI NCHINI ZAKABIDHIWA JIJINI DAR ES SALAAM NA MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wapili kulia), akimkabidhi tuzo, Makamu wa Rais wa kampuni ya Acacia, (Anayeshughulikia kampuni), Deo Mwanyika, baada ya mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni hiyo, kuibuka mshindi wa jumla wa mwaka 2014 wa tuzo ya Rais ya makampuni ya uchimbaji madini, yanavyotekeleza wajibu wa kampuni katika kusaidia jamii (CSRE). Hafla ya kutoa tuzo hizo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa muongozo mpya wa makampuni hayo katika kutekeleza CSRE. Aanayeshuhudia ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene        Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo, wakipiga makofi.
Makamu wa Rais, akimkabidhi tuzo, Meneja Ustawi wa Kampuni wa Mgodi wa North Mara, Abel Yiga, baada ya mgodi huo kuwa kinara katika migodi iliyomstari wa mbele katika kusaidia jamii, Kulia ni waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.Makamu wa Rais, akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa mgodi wa Buzwagi katika kusaidia jamii, Meneja wa Mgodi huo, Filbert Rweyemamu, huku waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akishuhudia. Makamu wa Rais, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Acacia.Wafanyakazi wa Acacia, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi wa jumla.
Mzee Mark Bomani, (kulia), akifurahia jambo na Meneja Ustawi wa kampuni, kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo.          Makamu wa Rais akitoa hotuba yake.Abel (kushoto), akibadilishana mawazo na Alex Lugendo, ambaye ni mshauri wa kampuni ya Acacia, katika mahusiano baina ya kampuni hiyo na serikali. Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akitoa hotuba yake. Makamu wa Rais, akimkabidhi tuzo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mine, (GGM). Makamu wa Rais, akizindua muongozo wa makampuni ya uchimbaji madini katika wajibu wao wa kusaidia jamii inayozunguka shughjuli zao za uchimbaji. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Waziri Simbachawene, Kamishna wa madini, Paul Masanja, na Afisa Mtendaji Mkuu, wa Jukwaa la wadau wa uchimbaji madini (EISF), Catherine Iyombe.Dkt. Bilal akimkabidhi tuzo ya Rais ya makampuni ya uchimbaji madini, yanavyotekeleza wajibu wa kampuni katika kusaidia jamii (CSRE), Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra-Tanzania, Frederick Kibodya. Anayeshuhudia ni Waziri wa Nishati nna Madini, George Simbachawene.

No comments: