ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 22, 2015

UKIINGIA KICHWAKICHWA BONGO MOVIES, UNAONDOKA NA ‘NGOMA’


Imelda Mtema
MSANII anayechipukia vizuri Bongo Movies, Suzan Odero ‘Taiya’ amefunguka kuwa kama mtu unaingia kwenye tasnia ya filamu kichwakichwa au bila kujitambua lazima uondoke na gonjwa hatari la Ukimwi (ngoma).
Msanii anayechipukia vizuri Bongo Movies, Suzan Odero ‘Taiya’.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Taiya alisema kuwa adha hiyo inawakuta sana wasanii ambao ndiyo kwanza wanataka kuingia kwenye tasnia ya filamu ili kufanikisha azma yao lazima watoe rushwa ya ngono ndiyo hapo wanapokutana na tatizo hilo.

“Jamani kama mtu siyo muangalifu utajikuta hupati nafasi ya kucheza filamu na ngoma umeibeba na kuhangaika nayo mitaani bila sababu yoyote,” alisema Taiya.
CREDIT:GPL

No comments: