JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA
KWA UMMA
YAH: UWASILISHWAJI WA MPANGO NA UKOMO
WA BAJETI KWA MWAKA 2015/16
_______________
Kesho Jumatano
tarehe 29 Aprili, 2015 Wabunge wote kwa ujumla wao watakutana katika Ukumbi wa
Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam kupokea Mapendekezo ya Mpango, Kiwango
na Ukomo wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/2016 kwa mujibu ya matakwa ya
Kanuni ya 97 ya kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2013.
Shughuli hiyo itaanza rasmi saa tatu na nusu asubuhi
kwa Waheshimiwa Wabunge na Washiriki wote kuwasili na kuketi Ukumbini kabla ya
ukaribisho utakaotolewa na Naibu Spika amabaye pia atakuwa mwenyekiti wa
Mkutano huo na kufuatiwa na neno la utangulizi kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe.
Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Aidha, Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango wa
Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 yatafanyika kuanzia saa nne asubuhi na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahususiano na Uratibu) Mhe. Dkt. Mary Nagu (Mb)
na kufuatiwa na uwasilishwaji wa mapendekezo ya kiwango na ukomo wa Bajeti ya
Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (Mb).
Shughuli hiyo inatarajiwa kumalizika saa sita
mchana, na baadae kamati za Bunge kuendelea na utekelezaji Majukumu yake
kulingana na ratiba za kamati.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
28 Aprili 2015
No comments:
Post a Comment