Advertisements

Saturday, April 25, 2015

Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka Balozi Mteule wa Urusi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Fedorovich Popov. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Urusi mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri aliishukuru Serikali ya Urusi kwa misaada inayotoa kwa Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile elimu. Wawili hao pia waliafikiana umuhimu wa kukuza na kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi. 
Mazungumzo yanaendelea. 
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania. 
Waziri Membe katikati akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Urusi. Wakwanza kulia ni Balozi Joseph Sokoine, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kutoka kushoto ni maafisa wa Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania. 

Picha na Reginald Philip.

No comments: