Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo
wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa
mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT). Kauli hii imekuja baada ya madereva wa mabasi yaendayo mikoani pamoja na
mabasi yanayofanya kazi ndani ya jiji la Dar es Salaam kugoma huku wakitaka
kuongea na viongozi wa juu wa serikalini ili kutatua tatizo lao.(Picha kutoka Maktaba)

2 comments:
Hii Serikali yetu vipi? Kama hii sheria ilianzishwa in a good faith iweje ifyate mkia kirahisi namna hii.walianza wamachinga,Leo madereva,serikali haioni ina set a wrong corse, kwani kesho utasikia waalimu,madaktari,police. ..yetu macho.
Jamani hii serikali yetu jamani inasikitisha mno.. I can not believe wamekubali wakati watau wanakufa kila siku .madereva wanatakiwa wapate somo upya ili waendesha kwa usalama.
Post a Comment