Advertisements

Monday, May 4, 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.

Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya kuwa naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizarani hapo.

Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015

Mwisho

Imetolewa ;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
4 Mei, 2015

3 comments:

Anonymous said...

Kwa niaba ya wabongo tunaoishi Virginia, tunakupongeza sana Mh. Balozi Mulamula kwa kupata nafasi hii muhimu katika Taifa, ni kweli unastahili. Hongera sana, BWANA YESU Kristo wa Nazareti akubariki sana na kukuongezea hekima, busara, nguvu na upendo mwingi katika maisha yako.

Anonymous said...

Nawauliza wadau wenzangu, jee hiyo ni "demotion" or "promotion"? kwani Kuwa katibu mkuu wizarani hakuna prestige kama kuwa Balozi Marekani! Besides, in seven months, Rais ajayo ataweka timu yake mpya. Haa! what is wrong with our country? Kwa nini tunabadilibadili mabalozi kila mara?

Anonymous said...

Anonymous 2: Kwa taarifa hiyo ni promotion kubwa na Rais ameona anafaa kuongoza Wizara ya Nje. Ni Mama mchapakazi sana hata Rais ajaye atamuhitaji sana.Viongozi wote Tanzania wanajua hilo. Amefanya kazi kubwa sana sehemu zote alizofanya kazi na ameacha historia. Hata Marekani ataacha historia. Mama kaongoze WIZARA wanakuhitaji sana.