Advertisements

Monday, May 25, 2015

Dakika tatu na Edward Lowassa>> Urais 2015, kuhama Chama, Elimu TZ.. Afya yake na Ujumbe wake kwa CCM



Moja ya story kubwa kwenye siasa za TZ wiki iliyopita ilikuwa ishu ya CCM kuwafungulia makada wake sita ambao walikiuka kanuni za chama hicho kwa kutangaza kugombea Urais mapema kinyume na utaratibu wa chama hicho, mmoja ya waliokuwa wamefungiwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Jana kulikuwa na stori ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba kutangaza kugombea Urais wa TZ kupitia CCM.. leo Mbunge Edward Lowassa ameongea kuhusu mambo kadhaa ikiwemo hali ya afya yake, chuki kwenye siasa, na ujumbe wake kwa CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 TZ.

Ishu ya chuki kwenye siasa >>”Kuna chuki imeibuka kwenye siasa za nchi yetu na kutakiana mabaya, afya ni neema kutoka kwa Mungu.. mimi niko sawa kabisa kwa chochote kile.. kwenye Chama chetu waweke utaratibu tukapimwe wote afya mimi nitakuwa wa kwanza kwenda kupima tuelezane nani mgonjwa“>> Edward Lowassa.

Sentensi yake nyingine kuhusu tatizo la ajira>>>”Tatizo la ajira ni bomu lisiposhughulikiwa.. toka nimetoka Serikalini kuna vitu ambavyo kama tungevifanya kwa kasi ile ambayo tulianza nayo ningepita napunga mkono nikapata kura zote, hatufanyi maamuzi iwe magumu au rahisi.. mambo yanakwenda legelege, Rais amefanya jitihada kubwa sana lakini kuna mambo hayaendi>>> Edward Lowassa.

Suala la elimu>>>”Tukiwekeza vizuri katika elimu tunaweza kubadilisha nchi yetu.. Tukitaka kuokoa nchi yetu tuwekeze kwenye elimu“>>> Edward Lowassa.

Kuhama CCM je? >>>”Kuhama chama sina mpango.. nimeingia CCM toka 1977 sijafanya kazi mahali pengine popote isipokuwa CCM.. My life is CCM.. huyo ambae hanitaki CCM ndio ahame sio mimi nihame“>>> Edward Lowassa.

Kauli yake kuhusu visasi >>> “Mimi ni Mkristo, ninaamini kwenye dini yangu sana… sina kisasi na mtu yoyote“>>>

“Upinzani umeanza kupata nguvu kubwa sisi ni chama dola tusibweteke.. wenzetu wanajiandaa vizuri na sisi tujiandae vizuri. Tusifanye mchezo tusibweteke”>>> MbungeEdward Lowassa.
Credit:Millard ayo.com

1 comment:

Anonymous said...

Asante sana mheshimiwa Edward. Tatizo kubwa sisi wana CCM ni hapa tulipowafikisha wananchi! Wewe mwenyewe ulikuwa kwenye serikali hii hii ambayo leo inatuambia inataka tutoe mtu safi atakayekubalika kwa wananchi. Bnafsi nimeamua kuachana na siasa. Mwigulu ni mwiba mwingine mkubwa saaana kwa taifa la Tanzania ni mzigo mkubwa bora basi wangekupa wewe tungeelewa kitu. Hakuna analoweza kulibadili Mwigulu kwenye serikali ile ile iliyomeza mamillion Escrow, mabehewa feki TRC, trillions zimeyeyuka kwenye ripoti ya CAG na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri amekiri hii ni aibu. TATIZO KUBWA NI Serikali ya CCM Inahitaji likizo. Vinginevyo hizo fedha zote zirejeshwe na hao waliosafishwa ni wasafi wasimame kazi wale waliotolewa kafara warejeshewe nafasi zao.Hii ni aibu tunazo rasilimali kibao tunashi9ndwa kuweka hata madawati mashuleni hadi wafadhili, kina majaar trust watoe madawati serikali iko wapi, fedha zinawekwa mifukoni kiholela tu. wafanyakazi wamekuwa wanaishi katika mazingira magumu mno! Miundo mbinu hovyo. Fedha za wanafunzi zinawekwa hadi waandamane ndio mzitoe waziri, naibu wake na wafaanyakazi wapo wanaokea mshahara kwanini wasizitoe hizo fedha tunatoa elimu gani kwa taifa la kesho?? Serikali na CCM kwa ujumla watueleze watanzania nini kipya wanachoweza kukifanya, MWIGULU sio mtaji pamoja na kudai alipelekwa kujifunza uongozi bado ni tatizo. WaTanzania umefika wakati maalumu wa kuchambua makapi na mbegu!! Asante.