ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 19, 2015

DAWASCO YAANZA NA OPERESHENI KATA MAJI KWA WATEJA WAO WENYE MADENI

SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM (DAWASCO) LINAHIMIZA WATEJA WAKE WOTE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM, MIJI YA KIBAHA NA BAGAMOYO KULIPA BILI ZAO KWA WAKATI NA KABLA MWEZI HAUJAISHA.

MTEJA ULIYETUMIA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA, NENDA  SASA KALIPIE KABLA HUDUMA HIYO HAIJASITISHWA NA WAKAGUZI WANAOPITA NYUMBA KWA NYUMBA.

ZOEZI LA USITISHWAJI WA HUDUMA YA MAJI LIMEANZA RASMI NA LITAHUSISHA WAKAZI WOTE WANAOHUDUMIWA NA DAWASCO.

KUMBUKA PINDI UTAKAPOSITISHIWA HUDUMA HII GHARAMA YA KURUDISHIWA NI TSH 15,000/= KWA WATUMIAJI WA MAJUMBANI NA TSH 50,000/= KWA TAASISI NA MAKAMPUNI. EPUKA USUMBUFU LIPIA HUDUMA HII SASA.

MALIPO YAFANYIKE KUPITIA NJIA ZIFUATAZO: 
M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, EZYPESA, CRDB, NMB, BARCLAYS, BOA BANK, MAXMALIPO NA SELCOM; AKIBA MOBILE, EXIM MOBILE, NMB MOBILE NA TPB POPOTE. 

LIPA BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE NA KWA WAKATI WOWOTE
KWA MAWASILIANO ZAIDI NAMBA YA HUDUMA KWA WATEJA 022-2194800, 0658-198889

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

DAWASCO MAKAO MAKUU

2 comments:

Anonymous said...

Maji yenyewe hayajatoka mwezi wanne sasa bili IPI sasa unayoingumzia uzembe mtupu hii operesheni ya nyumba kwa nyumba ingekuwa ya kwenda kuhakikisha kuwa wateja wanapata hiyo huduma na kukusanya maoni ili kuboresha hii huduma

Anonymous said...

Haaaaghaaaha operation kata maji??hivi hayo maji yenyewe yanatoka kweli bombani...hiki ni kichekesho kiingizwe kwenye maajabu ya dunia..lol