Adebayor ameamua kuandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Facebook akikana tuhuma ambazo amekuwa akitupiwa na ndugu zake huku akiweka wazi mambo yote mazuri aliyoitendea familia yake.
Staa huyo pia aliwahi kukana tuhuma alizotupiwa na dada yake kwamba alimfukuza mama yaka mzazi kwenye nyumba yake kwa tuhuma za ushirikina akieleza kuwa mama yake ndiye aliamua kuondoka kwenye nyumba hiyo.
Nilitunza habari hizi kwa muda mrefu ila leo ni muda muafaka wa kuziweka haradhani ili na nyinyi muweze kuzijua. Ni kweli kwamba mambo ya familia ni vizuri yajadiliwe kifamilia na si hadharani lakini nimeamua kufanya hivi nikiwa naamini kila familia inaweza kujifunza kutokana na yaliyonitokea.
Na ningependa wote mfahamu kuwa haya yote yalifanyika si kwa sababu ya fedha.
Nikiwa na miaka 17, kwa kutumia mshahara wangu wa kwanza kama mwanasoka, niliweza kujenga nyumba kwa ajili ya familia yangu na kuhakikisha wapo salama
Kama mjuavyo, nilitwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika 2008. Na nilikuja na mama yangu ukumbini na kumshukuru kwa mema aliyonitendea. Ndani ya
mwaka huo, nilimsafirisha mama yangu mpaka London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo mbalimbali vya kiafya.
Binti yangu alipozaliwa, tuliwasilina na mama yangu kumjulisha taarifa hizo ila baada ya kupokea simu yangu haraka aliikata na hakutaka tena kusikia habari kuhusu mwanangu huyo.
Nilipopitia maoni yenu, baadhi ya watu walisema kuwa mimi pamoja na familia yangu ni vizuri tukaenda kumuona T.B Joshua kwa ajili ya ushauri.
Mwaka 2013, nilimpatia mama yangu fedha ili aende kumuona T.B Joshua nchini Nigeria.
Alitakiwa kukaa Nigeria kwa wiki moja, ila baada ya siku mbili, nilipokea simu kwamba ameondoka.
Mbali na hilo pia nilimpatia mama yangu kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuanzisha biashara ya mapishi na bidhaa mbalimbali. Na niliwaruhusu kuweka picha na jina langu katika baadhi ya bidhaa ili kupata mauzo mengi. Sasa ni kitu gani kingine kijana afanye kwa ajili ya kuisaidia familia yake?
Miaka ya nyuma, nilinunua nyumba huko Lagon mashariki (Ghana) kwa dola milioni 1.2 na nikaona si vibaya kumuacha dada yangu mkubwa, Yabo Adebayor aishi katika nyumba hiyo.
Pia nilimruhusu kaka yangu wa kambo (Daniel) kuishi ndani ya nyumba hiyo.
Miezi michache baadaye, nikiwa likizo niliamua kwenda kwenye nyumba hiyo, cha kushangaza nilikuta magari mengi eneo hilo la nyumba. Bila shaka dada yangu aliamua kupangisha nyumba hiyo bila mimi kujua. Mbali na hilo pia alimfukuza Daniel ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa na idadi ya vyumba 15.
Nilipompigia simu ili anipe maelezo, aliamua kuniporomoshea matusi kwa takribani dakika 30. Nilipompigia mama ili kumueleza hali hiyo na yeye alinijibu kama alivyofanya dada.
Huyuhuyu dada anayesema sina shukrani, muulizeni kuhusu gari analoliendesha au biashara anazozifanya kwa sasa!
Kaka yangu Kola Adebayor, kwa sasa anaishi nchini Ujerumani kwa mwaka wa 25. Alisafiri kwenda nyumbani Togo mara nne kwa gharama zangu. Nilimlipia karo za masomo kwa ajili ya watoto wake. Na nilipokuwa Monaco, alikuja na kuniomba fedha za kuanza biashara. Mungu pekee ndiye anayejua kiasi gani nilimpatia. Je, biashara hizo ziko wapi leo?
Kaka yetu Peter alipofariki, nilimtumia fedha nyingi Kola ili aweze kusafiri kwenda nyumbani. Lakini hakuonekana katika mazishi.
Leo kaka huyohuyo (Kola) ndiye anayewaambia watu kuwa nilihusika katika kifo cha Peter. Kivipi? ndiye huyohuyo aliyekwenda na kueleza habari zisizokuwa za kweli kuhusu familia yetu kwa "The Sun". Pia waliwahi kutuma barua katika timu yangu nilipokuwa Madtid ili nifukuzwe klabuni hapo.
Nilipokuwa Monaco, nlifikiri ni vizuri kuwa na familia ya wanasoka, hivyo niliamua kumpeleka kaka yangu Rotimi ili ajiunge na akademi ya soka huko Ufaransa.
Ndani ya miezi michache, kati ya wachezaji 27, aliiba jumla ya simu 21.
Siwezi kumuongelea kaka yangu Peter maana kwa sasa ni marehemu. Roho yake ipumzike kwa amani.
Dada yangu Lucia Adebayor amekuwa akiwaambia watu kuwa baba yangu aliniambia nimlete Ulaya. Lakini sababu ya kumleta dada Ulaya ni nini? Kila mtu huku yupo kwa sababu flani.
Nilikuwa nchini Ghana nilipopata taarifa kuwa marehemu kaka yangu Peter alikuwa mahututi. Niliendesha gari kwa spidi kali iwezekanavyo kwenda Togo ili kumuona na kutoa msaada ambao ungehitajika.
Nilipofika, mama yangu alisema siwezi kumuona hivyo nitoe fedha na yeye atashughulikia kila kitu. Mungu pekee ndiye anajua kiasi gani nilimpatia mama kwa ajili ya matibabu ya kaka.
Watu wanasema sikufanya chochote katika kuokoa uhai wa kaka yangu, Peter. Je, mimi ni mpumbavu kuendesha gari masaa mawili kwenda Togo bila sababu?
Niliandaa kikao mwaka 2005 ili kutatua migogoro ya familia yetu. Nilipowauliza kuhusu maoni yao, walisema natakiwa kujenga nyumba kwa kila mwanafamilia na kumpatia kila mmoja mshahara wa mwezi.
Leo bado naishi lakini tayari wanataka kuendesha kila kitu changu, je, nikifa itakuwaje?
Kwa sababu zote hizo, itanichukua muda mrefu kuanzisha taasisi yoyote Afrika. Kila mara ninapojaribu kusaidia watu wenye uhitaji, wao lazima waniulize maswali huku wakiamini kuwa lazima liwe wazo baya.
Ninapoandika ujumbe huu, madhumuni yangu siyo kuweka wazi maisha ya familia yangu. Nataka familia nyingine Afrika kujifunza kutokana na yanayonisibu mimi.
ASANTE
Hivyo ndivyo alivyomalizia mwanasoka huyo raia wa Togo.
GPL
1 comment:
emannuel edebayor, muachiye mungu mungu anaona na mungu halali wala hasinzi,na atakulipa kwa wema wako wote ulio watendea familia yako na wao ndo walio kosa shukrani.watu wanatafuta ndugu katika familia kama wewe awasaidiye wao leo wanakukashifu.muachiye mungu atakulipa,malipo hapa hapa duniani,tenda wema uondoke.
sisi binadamu hata utufanyeje hatuna shukrani wala haturidhiki wanakuonea choyo tu kwa pesa zako na ni mafisadi sana hao familia yao na familia nyingi sana za kiafrica ndivyo zilivyo;na choyo cha roho.
wanafamilia wengi sana siku hizi wana thamini pesa kuliko utu wa mwenzake.muombe mungu akuepushiye mbali na nia zao mbaya kwako na mungu atakulipia.
mungu awe nawe daima milele na akukinge na shari zao zote na azidi kukubariki daimia amen.
kwakweli uliyonena yapo sana katika familia nyingi za kiiafrica.
from u.s.a
Post a Comment