
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akishirikiana na Wapigakura wake kushusha rola la Nyaya za umeme kwenye kijiji cha Luhana kata ya Luana wilayani Ludewa, jana Mei 18, 2015 kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini ambapo kijiji hicho pia kinatarajiwa kupata umeme hivi karibuni.


Mbunge jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akishirikiana na wapiga kura wake kushusha Transfoma kwa ajili ya kufungwa kwenye mradi wa umeme unaotekelezwa kwenye kijiji cha Luana wilayani Ludewa mkoani Njombe, jana Mei 18, 2015.
3 comments:
Kampeni nzurii sana mboa kama zingekuea zinafanywa kila mwaka wa kukaa kwenye uongozi mbona kila kijiji kingekuwa bora na maendeleo yangekuwepo. Baada ya chaguzi tunayeyuka. Daah uongozi wa aina yake..
nchi ya ajabu sana..hao wanaoshika vifaa vya umeme are they electricians or electric engineers?.au wanatafuta cheap publicity?
yaani miaka zaidi ya 50 ya uhuru huyo mbunge haoni aibu vifaa kama hivyo bado vinabebwa na watu badala ya machines?what has the Gov done kuondokana na hayo maisha ya ujima??mapesa yote yameishia kwenye ufisadi na kununua V8 then mnawadanganya wanavijiji kama hivi.
mdau
Texas
tusidanganyane! ni kujionyesha apate kura!
Post a Comment