ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 11, 2015

HUAWEI WANOGESHA BONANZA LA WAFANYAKAZI WA MABENKI MKOANI MBEYA

Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Lydia Wangari akizungumza na waandishi wa habari jana katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha TEKU mara baada ya kuzindua bonanza la wafanyakazi wa mabenki lililoandaliwa na Real Brand Solutions Ltd na kudhaminiwa na Huawei.
Baadhi ya wafanyakazi wa mabenki mkoani Mbeya wakipata huduma katika vibanda vya Huawei.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Huawei Mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini, Polyne Msuya (kulia) akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea banda hilo katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha TEKU jijini Mbeya ambapo Huawei ndiyo walikuwa wadhamini wakuu wa bonanza hilo. 
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Real Brand Solutions Ltd ambao ndiyo waandaaji wa bonanza hilo, Innocent Mafuru akiongea na wanahabari wakati wa bonanza hilo lililofanyika jana.
Timu za soka za wafanyakazi wa Benki ya Posta na Benki Kuu (BOT) wakimenyana katika bonanza hilo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya, Amani Kajuna (mwenye shati la mistari) akifurahia jambo na Polyne Msuya mara baada ya kutembelea banda la Kampuni ya Huawei kujionea simu za kisasa.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB na CRDB wakimenyana katika mpambano wa mpira wa kikapu.

No comments: