Sijawahi kuwa Mwanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo na sijafikiria kujiunga na chama hicho. Nilishawahi kuwa Mwanachama mtiifu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)
Nikiwa ndani ya CHADEMA nimewahi shiriki katika harakati nyingi zote zikiwa na lengo la kukikuza chama ambacho niliamini ndo mkombozi wa kweli wa mtanzania.
Bahati mbaya sikuwa sahihi, nilikosea kukiamini chama hicho ambacho idadi kubwa ya viongozi wake ni mahafidhina.
Nikiwa ndani ya siasa, nimefanikiwa kujuana na wanasiasa wengi wakubwa kwa wadogo, mmoja wao ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Namjua Zitto, nafahamiana naye vizuri, ni mmoja wa wanasiasa wasomi, wenye siasa safi ambaye mara zote kauli na hoja zake zimetaliwa na busara na nia ya kulijenga taifa, siwezi kusema si mbinafsi moja kwa moja lakini nina imani nae kubwa kuwa si mbinafsi.
Zitto ameweza kuzimudu siasa safi za taka zilizokuwa zikiendeshwa ndani na nje ya chadema kabla ya kuhamia ACT- Wazalendo.Ameweza kupambana na kupenya kwenye changamoto nyingi za kisiasa hasa siasa hizi za kuwa na chama kimoja kikongwe na chenye nguvu nchini na nje ya nchi.
Sote tunaijua CCM ni chama chenye wanachama na viongozi wanaoijua siasa, wanaweza kukibadili chama hicho wakati wowote, chama hiki kikuu nchini ni kama kinyonga, kinabadiilika kulingana na mazingira na wakati.
CCM kinapanga vyema karata zake, kina propaganda zenye kuwiana na ukweli tofauti na ilivyo kwa upinzani ambao wanadanganya wananchi mpaka wanajidanganya wao wenyewe.
Zitto ameweza kupenya kote huku na ndio maana leo hii, Zitto anaposulubiwa hata CCM kinaumia na kumhurumia, kwa sababu wanamjua mwanasiasa huyu kijana ni mtu wa namna gani.
Kama si uimara wa Zitto huenda angeshaanguka maana wapo watu na vyama vilivyotupwa nje ya siasa kutokana na kukosa misingi ya mapambano ya siasa za aina zote.
Hata hivyo chadema kimefika hapo kilipo pamoja na mambo mengine mchango wa Zitto unahusika kwa kiwango kikubwa.
Katibu mkuu wa chadema Dr. Wilbroad Slaa kwa kushirikiana na Zitto walieweza kukifikisha chama hapo kilipo, hilo haliepukiki na anayekataa ana chuki zake binafsi.
Zitto akiwa mchanga kisiasa lakini mwenye maono alichanga karata zake vyema, akashiriki kukitoa chama kutoka kuwa na wabunge 11 hadi kukifikisha hapa kilipo, ambapo leo kuna zaidi ya wabunge 40.
Historia ya Chadema haiwezi kukamilika bila ya kumhusisha Zitto katika mafanikio yake huku akipambana kwa karibu sana na Dr. Slaa, na mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye kwa bahati mbaya amejikuta akivurugwa na wapambe.
Chadema ya Zitto akiwa kama Naibu katibu mkuu Bara, waliweza kukidhibiti CUF na Hamad Rashid ambaye alikuwa kinara ndani ya bunge.
CUF ilikuwa na hoja dhaifu na mikakati isiyotekelezeka pamoja na kauli mbiu za hatari za mapanga shaa,Interehamwe na Saigon.
Chadema ya Zitto na Dr Slaa walikuwa wakitoa hoja zenye mashiko, walikuwa moto mkali ndani ya bunge, hakuna aliyeacha kuwasikiliza watu hao wanapopata nafasi ya kuzungumza.Bunge la 9 lilikuwa ni moto wa kuotea mbali.
Bunge hilo lilileta mapinduzi makubwa ya kiungozi na kiutendaji serikalini.Mikataba mibovu ilichambuliwa,Sakata la EPA iliiibuka, mgodi wa Buzwagi nao ulipewa nafasi na masikini walipiganiwa.
Chama kikanawiri na kushamiri hadi kufikia leo kuwa na wabunge 40, ajabu ni kwamba baadhi ya viongozi wa chama hicho wamesahau mema yote ya Zitto badala yake wanashiriki kwenye harakati chafu za kumchafua.
Wanataka kuiaminisha jamii kuwa Zitto ni Msaliti, kwamba anapaswa kutukanwa, kusimangwa na kubezwa. Zitto huyu anayejua kupanga karata leo hii amekuwa adui na msaliti wa chadema, chama alichojiunga nacho akiwa kinda!
Dhambi hii ya ubaguzi waliyoifanya Chadema itawarudia, hawatapona kamwe, hawatabaki salama, wataparanganyika tu, nawaombea heri wasifike huko ingawa dhambi ya ubaguzi haiishi.
Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, namjua Zitto, nimefanya nae kazi ni mmoja wa waliokuwa viongozi kipenzi cha watu wa rika na kada zote ndani ya chama hicho.
Alipendwa naa viongozi wa ngazi ya chini Chadema, alikuwa ni mtu wa kujishusha na kuwasikiliza viongozi waliochini yake.Hata kama aliyoelezwa yalikuwa nje ya uwezo wake hakuyapuuza.
Tofauti yake na viongozi wakubwa wa chadema, yeye alikuwa akifika kwenye mikutano hata akute watu wachache hakuwa akiacha kuhutubia na kuwapa moyo.
Alikuwa akiyatumia mazingira hayo ya watu wachache kusimulia baadhi ya visa vyake vya kisiasa, wakati huo ndo wanajenga chama.
Naamini anakikumbuka kisa hiki, kwamba yeye na Mdee walikwenda mahali na kukuta watu wachache.Hwakuacha kuhutubia, walihutubia, lakini ajabu hao watu wachache waliokuwepo walikuwa wakiendelea na harakati zao, wengi wao walikuwa wakinunua ndizi mbivu......Kwa maana nyingine hawakuwa wakisikilizwa.
Alichokifanya ni kumuomba Mdee akazinunue zile ndizi zote ili watu wakose cha kununua na badala yake wageuke kuwasikiliza.
Hata hivyo, mpango wao huo haukufanikiwa, kwani kila mtu aliyekuwa pale aliendelea na mambo yake. Chakufurahisha Zitto na Mdee hawakukata tamaa, walipambana kuwashawishi watu wakielewa chama.Leo hii chama kikifika eneo lile lile watu wanakanganyana ili kumsikiliza kiongozi wa chama anayezungumza hata kama anaongea pumba.
Zitto alikuwa mtu wa kujichunga sana katika matamshi yake, hakuwa akiongea bora aongee, alikuwa akiongea yanayopaswa kuongelewa kwa wakati huo na kwa wakati stahiki.
Mwandishi: Joseph Yona ( 0713802226)
1 comment:
Mkuu, naona unafanya propaganda za kumtetea Zitto. Nadhani umechelewa kwa hili, Zitto has moved on na Chadea pia. Nashangaa wewe ndo bado unalilia hapa, hii ni opinion yako jinsi unavyomfahamu Zitto, what about watu wengine waliomuweka ktk siasa wakati akiwa pale UD na kumuwezesha kuwa mbunge? Wanamfamu vipi?. Pengine ungechunguza zaidi kabla ya kuandika hii article, may be Yule Zitto uliyemjua kabla ya kuwa na kitu sio Zitto wa Leo!. Remember watu wengine wanaweza badilika kutokana na circumstances, so wewe una hakika gani Zitto sio one of them? Waenga walisema, lisemwalo lipo na Kama halipo laja. Suala la Zitto kuwa msaliti sio la kupakaziwa kama wewe unavyodai, tafuta evidence utaonyeshwa kuwa jamaa yako anaubinafsi sio kidogo but kwa sana.
Post a Comment