Advertisements

Tuesday, May 5, 2015

KUNA WANAOISHI KWA RAHA NA VIMADA KULIKO NDANI YA NDOA


Nisiku nyingine tena tunakutana katika jungu kuu lisilokosa ukoko, katika uchambuzi mzuri na wenye mashiko kuhusu maisha na mapenzi.Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya kwa kuzungumza na wanaume kadhaa walio kwenye mahusiano, (hasa wana ndoa) nimegundua baadhi ya wanaume wamejikuta wakijiingiza katika masuala ya ulevi na kuchepuka (kwa kuwa na vimada) kwa sababu ya karaha wanazokutana nazo kwa wake zao.

Nilichobaini wanaume wengi wanaishi kwa raha mustarehe na vimada wao kuliko ndani ya ndoa zao. Sihalalishi kuchepuka wala kuwa na kimada ila huo ndiyo utafiti nilioufanya.Kiasili wanaume ndiyo watafutaji wa mahitaji muhimu ya kila siku ya familia, jambo linalowafanya kukutana na misukosuko mingi ya kila aina ikiwemo ugomvi, ushirikina, matusi, vishawishi n.k.

Hujitahidi kuvumilia misukosuko hiyo ili kuhakikisha anapata mkate wa siku hiyo, ili kutunza familia yake nakuendelea kuheshimiwa na watoto hata majirani kama baba mwenye kujali.Ishu inakuja pale mwanaume anaporudi nyumbani akitegemea kupokewa na mke wake kwa furaha, bashasha ili zimpoze na uchovu wa kazi alionao, lakini hali huwa si kama anavyotegema zaidi ya kukutana na karaha kutoka kwa wanawake wao.

Wakati mwingine mwanaume hutoka kazini mapema ila kila akifikiria makelele na karaha za nyumbani, basi anaamua kukata kona kwenye baa ili angalau apoteza muda wa kurudi nyumbani akute mkewe amelala.

Kwa mazingira hayo huoni kama hilo ni tatizo? Hebu jiulize wewe mke, mara ya mwisho ni lini umechukua mkono wa mumeo na kuushikisha kwenye kiuno chako huku mkitazamana kwenye kioo, jaribu kukumbuka mara ya mwisho kumbusu mumeo ilikuwa lini.

Kama ulikuwa hujui vimada kwa sehemu kubwa wanacheza na fursa, wanajua kuzitumia ipasavyo.
Udhaifu wako dhidi ya mumeo ndiyo mafanikio ya kimada, anachofanya yeye ni kutumia ule udhaifu wako uliomfanya mumeo akachepukia kwake, yawezekana umeifanya ndoa yako kuwa ya mazoea, humpetipeti tena mumeo kama zamani.

Haumfanyii mambo mazuri kama enzi za uchumba, umtumbui chunusi kama mlivyokuwa mnatongozana na badala yake umegeuka Manny Pacquiao au Mayweather ndani ya nyumba, badilika mama!
Tukutane wiki ijayo katika mada nyingine nzuri zaidi.

GPL

No comments: