Advertisements

Saturday, May 30, 2015

Mapishi ya bagia na chatney ya machicha ya nazi


Mahitaji
Kunde (Ila mimi nilitumia Nigerian brown beans 1/2 kilo)
Vitunguu maji (onion 2)
Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
Vitunguu swaum (garlic 4 cloves)
Chumvi (salt)
Barking powder (1/2 kijiko cha chai)
Machicha ya nazi (grated coconut 1 kikombe cha chai)
Limao (lemon 1)
Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Loweka kunde usiku mzima kisha ziondoe maganda na uzitie kwenye blender pamoja na vitunguu maji, vitunguu swaum, pilipili, chumvi,barking powder na maji kiasi. Visage vitu vyote mpaka viwe laini na kisha uutoe na kuweka kwenye chujio ili uchuje maji. baada ya hapo zikaange katika mafuta mpaka ziwe za brown na uzitoe na kuziweka kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta.Baada ya hapo saga machicha ya nazi,limao, pilipili chumvi pamoja na maji kidogo na hapo chatney yako itakuwa tayari kwa kuseviwa na bagia.

1 comment:

Anonymous said...

pia unaweza kujaribu kusaga kunde bila baking powder ziache for at least six hrs zitaumuka zenyewe, pia chuja maji kabla ya kusaga kunde ili kusave vitamins, ukichula baada ya kusaga unaondoa virutubisho. That's just my way of making bagia. Good recipe thanks!!!