Advertisements

Thursday, May 28, 2015

Marekani:Jeshi latuma Kimeta kimakosa


Maafisa 22 waliogusana na zana hiyo ya kimeta katika kambi ya Osnan Korea Kusini wanachunguzwa

Maafisa wakuu katika idara ya ulinzi ya Marekani wamekiri kuwa chembechembehai za ugonjwa hatari wa Kimeta zilitumwa kimakosa kwa kambi 9 za kijeshi nchini Marekani na moja nchini Korea Kusini.
Kulingana na makao makuu ya ulinzi nchini Marekani sampuli za chembechembehai za Kimeta zilidhaniwa kuwa zimekufa na hivyo zikatumwa kutumia njia ya usafirishaji mizigo ya umma kimakosa.

Chembechembe hizo za kimeta zilikuwa zimenuiwa kutumika katika mazoezi ya shambulizi la zana za kibaiolojia zakijeshi katika kambi za mazoezi.

Wandani wa maswala ya zana za kibayolojia wanasema kuwa kungetokea maafa makubwa iwapo chembechembe hizo za kimeta zingeachiliwa nje ya maabara maalum ya kibayolojia.

Maafisa wa serikali ya Marekani walioko Korea Kusini wameripoti kuwa takriban watu 22 waliogusana na zana hiyo katika kambi ya kijeshi ya Osnan wanachunguzwa.Kimeta ni hatari ikinuswa au ikiliwa.

Hadi sasa hakuna kati yao aliyeonesha dalili za maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

Wakati ukweli ulipobainika mahabara na vituo vya kijeshi vilifungwa.

Kimeta ni hatari ikinuswa au ikiliwa.

Ni silaha inayoweza kutumiwa wakati wa vita vya kemikali.

No comments: