Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya tano ya Sekta ya Makazi kwa mwaka 2015 Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi, Julius Ndege, Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Amani Majula waandaaji wa maonyesho hayo, Ofisa Masoko wa EAG Group, Helen Mangare na Richard Ryaganda, Ofisa Masoko wa EAG Group.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya kufungua maonyesho hayo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Amani Majula.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Amani Majula (katikati), akiteta jambo na DC Makonda (kushoto) na Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi, Julius Ndege.
Ofisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (N.H.C), Vicent Ngaile (kulia), akimuelekeza jambo DC Makonda baada ya kutembelea banda la shirika hilo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco Village, Ahzari Marik (kulia), alipotembelea banda la kampuni hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masaimara Gardening, Murwa Kihore Simindei (kulia), akizungumza na DC Makonda alipotembelea banda lao.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ivan Amulike (wa pili kushoto), akimuelekeza jambo DC Makonda katika maonyesho hayo. Wa nne kulia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Tumaini Iddi Setumbi na kushoto Ofisa Ardhi, Brenda Kuringe. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment