ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 28, 2015

Mwandosya kutangaza nia ya urais Jumatatu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kutangaza nia ya kugombea urais Juni Mosi na kuchukua fomu Juni tatu mwaka huu.

Mwandosya ambaye tayari ametangaza kuacha kuwani ubunge katika jimbo la Rungwe Mashariki, anakusudia kuchukua fomu siku hiyo kuwania mbio za urais.

Profesa Mwandosya alisema sababu zilizomsukuma kuwania urais, atazitaja Juni Mosi atakapotangaza nia mkoani Mbeya.
Alisema Sababu za kutaka kuwania urais na nini nitawafanyia watanzania, akiingia madarakani ataeleza siku ya kutangaza nia Juni Mosi.

Waziri Mwandosya ni mmoja kati ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao kwa muda mrefu wameonesha nia ya kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake.

Waziri Mwandosya aliwahi kuwania urais mwaka 2005 na kushika nafasi ya tatu akiwafuatia Dk. Salim Ahmed Salim na Raos Jakaya Kikwete aliyeibuka mshindi.
 

CHANZO: NIPASHE

3 comments:

Anonymous said...

Mgonjwa au kapona.

Anonymous said...

Cancer huwa haiponi..!

Anonymous said...

Nani kasema cancer huwa haiponi? Cancer ya namna gani hiyo?