Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), limetimiza ndoto za Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, za kuwa mwenyeji wa michuano mikubwa baada ya juzi kuipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Katika michuano hiyo, Tanzania itashiriki michuano hiyo bila kupita katika hatua ya mchujo kutokana na faida ya uenyeji, ambao pia utatoa fursa ya kuomba kuandaa michuano mikubwa ya Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF juzi usiku, katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizo Tanzania, Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano hayo wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za 2019.
"TFF inamshukuru Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara, kwa kufanikisha uamuzi huu, na inaamini ushirikiano huu wa serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya 2019," ilisema taarifa hiyo.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment