Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Samunge Social Research Centre, George Nyaronga (katikati), akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kuhusu viongozi wanaotaka kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameonesha kuwapiku wenzake kwa kupata asilimia 20 akifuatiwa na Dk.Willibrod Slaa aliyepata asilimia 11.7. Kushoto ni Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Wakili Mambo na kulia ni Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Gideon Anyona kutoka Chuo Kikuu cha Kenyata.
Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
NYOTA ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa yazidi kung'aa baada utafiti uliofanywa na Samunge Social Research Center na kugundua wananchi wengi kumpenda na kumuhitaji agombea urais wa mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mtafiti Mkuu wa Tafiti hiyo George Nyaronga alisema baada ya Waziri huyo kudai kuwa atagombania wananchi wengi wameonyesha kumuhitaji kwa kiasi kikubwa.
Alisema katika utafiti huo walioufanya waligundua kuwa Waziri huyo mstaafu anaongoza kwa asilimia nyingi kuliko wenzake anaowafata.
Akitaja asilimia hizo alisema Edward Lowassa anaongoza kwa asilimia 20.7 akifuatiwa na Wilbroad Slaa asilimia 11.7, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema)Freeman Mbowe asilimia 3.4, Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi CUF Ibrahim Lipumba asilimia 4.2.
Wengine ni pamoja na Waziri wa Ujenzi John Magufuli 7.6, Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba asilimia 4,Waziri Mkuu Mizengo Pinda asilimia 2.4,Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Bernard Membe7.0 na Mwenyekiti wa chama cha Nccr Mageuzi James Mbatia 1.2.
Alisema kwa kutokana na nchi kuelekea katika uchaguzi wananchi wamekuwa na muamko wa hali ya juu katika kuhakikisha kila mmoja atapigapiga kura kwa mwaka huu.
"Tumefanya tafiti hizi na kuona kwamba watanzania wengi wameamua kuingia kwenye masuala ya siasa na kuleta mabadiliko katika nchi yao na si kupigiwa kura,"alisema.
Alisema kutokana na utafiti wao wamegundua kuwa wananchi wanahitaji rais ambaye ni muadilifu, msema ukweli, mwenye afya asiwe na udini wala ukabila na mzalendo wa nchi yake
Alisema kutokana na majina hayo ya urais pia katika tafiti zao imeonekana kuwa vyama vinavyoongoza katika kupendwa na wananchi ni pamoja na Chama cha Mapinduzi kuonekana kupendwa sana kuliko vyama vyote.
Alivitaja vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) 53.5,Chama cha Demokrasia (Chadema) 34.2 ,Chama cha Wazalendo (ACT)1.2 na Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa) 6 na Chama cha wanachi CUF 6. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
4 comments:
Inasikitisha kuona hata tathmini za wagombea urahisi zinafanywa na raia wa Kenya kwa kupitia kampuni zao wanazoiita ni za research hivi hakuna wazawa tunayoijua nchi yetu na kuwajua viongozi wetu na kujua hali halisia ya nchi yetu pamoja na viongozi wanaotaka kuwania kiti cha urais 2015 tukafanya huo utafiti mpaka ufanywe na watu ambao sio wazawa na they know nothing about our country more than to make money na kuondoka kweli Tanzania Uzelendo umetuishia sijui tunakwenda wapi
tunapokwenda kwenye ufisadi because thats the game of the day.kila mtu roho imemtoka kwa pesa pesa hakuna hata kujali ikiwa ya haramu ndo tamu sana ikiwa ya halali haina utamu.vijana wazee wote wanapenda ufisadi hakuna uzalendo tena .wageni ndo wenye mamlaka ya nchi hii kuliko wazawa. back tanganyika yetu back
Tanzanians are lazy people.
hakuna mkenya hapo hata mmoja....wabongo hao. kusoma kenya ndo uwe mkenya....shenzi type.
Post a Comment