ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 12, 2015

Rais Kikwete azuru Maeneo ya Mafuriko Dar-Ajionea Uharibifu

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekagua baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya na mafuriko jijini Dar es Salaam na kuwapa pole wakazi wa maeneo hayo..Maeneo Aliyotembelea Rais leo ni Mbagala Mwanamtitu na Daraja la Msimbazi ambapo amejionea uharibifu uliofanywa na mvua zinazoendelea kunyesha.Pichani Rais Kikwete akiangalia Darala la Mwanamtitu Mbagala lililosombwa na maji na daraja la muda la miti lililojengwa na wakazi wa Eneo hilo na kisha kuwapa pole kwa adha wanazozipata
Rais Dkt..Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la mto Msimbazi Eneo la Jangwani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo.

.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa mhandisi wa TANROADS kutoa uchafu ulijaa chini ya daraja la Msimbazi eneo la Jangwani
Picha na Freddy Maro

4 comments:

Anonymous said...

HIVI MPAKA RAIS ATOE MAELEKEZO KUWA UCHAFU UTOLEWE CHINI YA DARAJA? INA MAANA HAO WENYE KAZI ZAO HAWALIONI HILO?

Anonymous said...

Rais profesa dakta Kikwete ni ENGINEER???ha ha ha yaani bongo inafurahisha sana kitu kipo wazi kuwa uchafu ukiziba maji hayapiti lakini ma-engineer wa kibongo hawaoni mpaka mh rais akawaambie!.ha ha dah kazi sana

mdau

singapore

Anonymous said...

Hahaha hahaha!!,cha ajabu hawajaribu kuzuia chanzo cha tatizo utupaji ovyo wa taka especially mifuko ya nailoni,common sense haitaji udaktari,kila siku kutembelea waanga wa mafuriko ni kama mchezo wa kuigiza.

Jay said...

Hapa wabongo tukiitwa au kubatizwa wajinga na majirani zetu mapovu yanatutoka. This is pure common sense, uchavu kwenye mitalo huzuia maji kwenda yanapostahili ila raia hawalioni hili kisingizio eti serikali ndiyo wenye mamlaka ya kutoa taka mitaloni, ni kweli jamani?