Advertisements

Thursday, May 28, 2015

SALAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA TAWI LA CCM NEW YORK


Kufuatia kifo cha kada wa muda mrefu wa Chama cha Mapinduzi na kiongozi mstaafu wa serikali mzee wetu Samuel Luangisa kilichotokea tarehe 05/25/2015 mjini New York, Marekani. Chama Cha Mapinduzi tawi la New York na vitongoji vyake inaungana na familia ya marehemu mzee Luangisa na watanzania wote kuomboleza msiba huu mkubwa. Tunatoa rambirambi zetu kwa familia yake hapa Marekani, nyumbani Tanzania na watanzania wote. Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amen.
Imetolewa na
Uongozi CCM tawi la New York na vitongoji vyake.

No comments: