Advertisements

Thursday, May 28, 2015

SEVILLA YATWAA KOMBE LA EUROPA

Carlos Bacca akiifungia Sevilla bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 73 ya mchezo.
Sevilla wakishangilia ubingwa wao baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Dnipropetrovsk.
Washindi wa Kombe la Europa mara mbili mfululizo wakiwa katika pozi baada ya ushindi.


TIMU ya Sevilla ya Hispania imefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi ya Europa baada ya kuichapa Dnipropetrovsk ya Ukraine mabao 3-2.

Mabao ya Sevilla katika mechi hiyo iliyopigwa jana usiku mjini Warsaw nchini Poland yaliwekwa kimiani na Carlos Bacca aliyetupia mawili na lingine likifungwa na Grzegorz Krychowiak huku ya Dnipropetrovsk yakifungwa na Nikola Kalinic pamoja na Ruslan Rotan.

Sevilla wamechukua kombe hilo mara ya pili mfululizo baada ya kulitwaa pia mwaka 2014.

No comments: