ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 29, 2015

SERIKALI YAPANIA KUMCHUKULIA HATUA SHILOLE

Serikali imeahidi kumchukulia Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Akizungumza bungeni Dodoma jana, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia

“Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,” alisema Juma Mkamia.

5 comments:

Anonymous said...

Nafikiri ingekuwa vyema serikali ikajikita kushughulikia mikopo ya wanafunzi, ukosefu wa vitanda vya wajawazito hospitalini, ujenzi wa madaraja, mafuriko Dar, ukosefu wa umeme, ukosefu wa maji, ukosefu wa vyakula mashuleni, upungufu wa maabara shule za kata, upungufu wa walimu shule za kata, upungufu wa madawa hospitalini, msongamano wa takataka Dar, ukosefu wa ajira kwa vijana/wasomi, polisi kutumia nguve bila akili, majambazi, ukosefu wa vitabu mashuleni, umaskini uliokithiri, vistula pamoja na majanga mengine ambayo ni kero kwa wananchi. Kutumia kodi za wananchi kumjadidili Shilole ni umaskini wa akili. Mbona kina dada wa kimasai wanatembea matiti nje na hawajadiliwi bungeni????????

Anonymous said...

Baelezee wanafikiri kwa makalio hawa

Anonymous said...

well said mdau wa mwanzo hapo juu.na kidogo kuongezea wanao uza sembe list mnayo mbona hamtoi mnawakamata vipunda vinavyobeba hiyo sembe. escrow,richmond mbona mmenyamazia kimya. watanzania wa sasa si wajinga.

Anicetus said...

mheshimiwa Anonymous - list yako ni ndogo. Wanaotakiwa kulalamika ni Wabeljiji na sio bunge au serikali ya Tanzania. Huyu msanii- Shirole amelipwa kwa dola au euro na anazitumia hizo pesa nchini Tanzania- anongeza uchumi wa nchi yetu. Viongozi wajielimishe zaidi maisha ya wakati wa sasa.

Anonymous said...

Wewe mdau hapo juu, una akili sana, mijitu inakaa bungeni kula hela za wananchi kujadili upuuzi, halafu kwa pembeni wanamtafuta malaya mtaani wakulala nae, hospital hazina dawa, wa2 wanakufa, nyie mnataka kumjadili shilole..pumbafu zenu.