ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 11, 2015

SHIGONGO AZINDUA VITABU VYAKE VITATU VIPYA KATIKA OFISI ZA GLOBAL

Mkurugenzi wa Global Publishers LTD, Shigongo Eric James (kulia), akishikilia vitabu vyake baada ya kumpatia jukumu la uzinduzi huo Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Kampuni hiyo, Oscar Ndauka. Tukio hilo limefanyika mapema leo ndani ya jengo la ofisi za GlobalPublishers zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia), akiwa amenyanyua moja ya vitabu hivyo baada ya zoezi la kukata utepe wa uzinduzi kukamilika.  Katikati ni mtunzi wa kitabu hicho, Shigongo Eric James na Oscar Ndauka, wote wakiwa wamenyanyua vitabu hivyo. Vitabu vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni  ’26 Secrets – How to Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.

Shigongo akimkabidhi jukumu la kukata utepe Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa Oscar Ndauka (wa kwanza kushoto) huku Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Abdallah Mrisho anashuhudia zoezi hilo.
Shigongo akiwaonyesha mojawapo ya vitabu hivyo baadhi ya wanahabari waliokuwa wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo (hawapo pichani).
Shigongo akiongea machache kwenye uzinduzi huo.
Baadi ya wanahabari kutoka sehemu mbalimbali wakichukua matukio ya uzinduzi huo.
Shigongo akisisitiza jambo juu vitabu hivyo kwenye uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, akiwakaribisha wanahabari katika uzinduzi huo.
Afisa Masoko wa Global Publishers Ltd, Benjamin Mwanambuu, akiongea jambo na waandishi wa habari kabla ya zoezi la uzinduzi huo kuanza.
Wanahabari wakiwajibika.
Shigongo akisaini moja ya vitabu hivyo tayari ya kukitoa kama zawadi kwa baadhi ya wanahabari walioshuhudia uzinduzi huo.
Mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo akisainiwa kitabu alichopewa.
Baadhi ya waandishi na wahariri wa Global Publishers Ltd wakisainiwa vitabu hivyo.
Shigongo akisaini kitabu kimojawapo.
MHAMASISHAJI na mjasiriamali wa kimataifa, Eric James Shigongo, amewaasa Watanzania kutokata tamaa katika kufuatilia ndoto zao huku wakiamini kuwa wao ni watu muhimu katika maisha yao na ya jamii.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo ndani ya ofisi za Global Publishers zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar katika uzunduzi maalumu wa vitabu vyake vitatu, Shigongo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kusoma vitabu ili kupata maarifa mengi ya juu ya mafanikio maishani.
 “Kila mmoja ana ndoto za kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kuondoka mahali alipo. Wengi hushindwa kupiga hatua za mafanikio maishani kwa sababu nyingi yakiwemo mazingira waliyokulia wakiaminishwa kuwa hawawezi kufanya chochote maishani,  jambo ambalo si la kweli kwani kila mmoja anaweza kufikia ndoto zake akiamua tu kubadili fikra na namna ya kutenda mambo maishani,” alisema Shigongo.
Vitabu vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni  ’26 Secrets – How to Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.
Uzinduzi wa vitabu hivyo ni kuashiria kwake kuingia rasmi mitaani na kusambazwa kwenye kona mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo vinatarajiwa kubadilisha maisha ya maelfu ya wasomaji watakaofanikiwa kupata siri za mafanikio.
(PICHA: MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS/GPL)

No comments: