ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 12, 2015

SHULE YA SEKONDARI MTAKUJA YA KUNDUCHI BEACH, DAR, YAPOKEA MSAADA WA KOMPYUTA TOKA VODACOM FOUNDATION

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi beach jijini Dar es Salaam, wakishusha vifaa vya kompyuta mpakato kwa kushirikiana na maofisa wa Vodacom Tanzania, Jumla ya kompyuta(25) pamoja na vifaa vingine vimetole msaada na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung na vitafungwa hivi karibuni kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza akiwapa maelezo wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja juu ya utumiaji wa kifaa maalumu cha kuhifadhia na kuchajia kompyuta mpakato.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika shule ya sekondari ya Mtakuja, Elizabeth Claud akibofya komputa mpakato wakati Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza alipokuwa akiwaonyesha kompyuta hizo.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza,akifurahia jambo pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja.
Kompyuta mpakato 25 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation kwa ushirikiano na Kampuni ya Samsung katika shule ya sekondari ya Mtakuja zikiwa zimehifadhiwa katika kifaa maalumu cha kuhifadhia na kuchajia Kompyuta hizo.

No comments: