ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 29, 2015

TANGULIA KWA AMANI SHEIKH OMAR ALHADY ULIYEDUMU SIKU 10 TU MADARAKANI!


Sheikh Omar Alhady

Mwenyekiti mpya wa Villasquad, Sheikh Omar Alhady amefariki dunia juzi katika hospital ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la figo.
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi aliongoza mazishi yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
Sheikh omary alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu katika mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika mwezi huu tarehe 17 na amedumu kwa siku kumi tu (10) tangu achaguliwe.
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Allu Hassan Mwinyi akiwasili katika msikiti wa kichangani kuaga mwili wa mwenyekiti wa Villasquad, Omar Alhady

Enzi za za uhai wake Sheikh Omary alikuwa mmoja wa Masheikh mashuhuri nchini .Pia alikuwa Imàm katika msikiti wa kichangani.
Klabu ya Villa wamepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa na hatuwa jinsi, wamebaki wameduwaa.

Villa wanatoa pole kwa familia ya marehemu. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Taarifa na Iddi Godigodi 
Mkurugenzi wa Mawasiliano Villasquad.
Credit:SHAFFIHDAUDA

No comments: