Advertisements

Friday, May 22, 2015

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUANZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU WAPIGA KURA RASMI KWA MFUMO WA BVR MKOANI KAGERA KUANZIA MEI 21 HADI JUNI 18, 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuzindua rasmi uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa (Biometric Voters Registration BVR) mkoani Kagera katika Manispaa ya Bukoba kesho tarehe 21/05/2015 kuanzia asubuhi saa mbili. 

Zoezi la uzinduzi litaongozwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella katika mtaa wa Pwani eneo la uwanja wa ndege wa Bukoba kata ya Miembeni Manispaa ya Bukoba. Uzinduzi huo utafanyika katika Halmashauri zote za wilaya siku hiyo ya kesho Halhamisi na kuanza uandikishaji rasmi katika mkoa wetu wa kagera. 


Kulingana na ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uandikishaji wa wananchi katika mkoa wa Kagera utafanyika kwa siku 29 kuanzia hiyo kesho Mei 21, 2015 hadi Juni 18, 2018 ambapo maoteo ya uandikishaji ni wananchi 1,217,388 kwa mkoa wa mzima. 


Wananchi wanaotarajiwa katika Halmashauri hizo ni 92,000 Bukoba Manispaa, Bukoba 148,033, Biharamulo 150,000, Karagwe 130,000, Kyerwa 150,000, Missenyi 144,600, Muleba 198,600 na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ni 128,000. 


Aidha vituo vya uanduikishaji vilivyoainishwa katika mkoa mzima wa Kagera nia 1,676 ambapo Bukoba Manispaa ni vituo 75, Halmashauri ya Bukoa 250, Biharamulo 140, Karagwe 217, Kyerwa 207, Missenyi 174, Muleba 395, na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara 218. 


Wananchi wa Mkoa wa Kagera wote wanaokidhi vigezo pia wenye umri wa miaka 18 wanahamasishwa kujitokeza katika vituo vitakavyokuwa katika maeneo yao kujiandikisha ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba mwaka huu.

No comments: