ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 12, 2015

VIONGOZI WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA JOHN NYERERE

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu John Nyerere.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha rambi rambi kwenye msiba wa John Nyerere
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kwenye msiba wa John Nyerere ambapo viongozi mbali mbali walijumuika kutoa heshima za mwisho.
Makama Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye msiba wa John Nyerere .
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonyesha jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)Philip Mangula kwenye msiba wa John Nyerere ,msasani jijini Dar es salaam.(Picha na Adam Mzee)
Makongoro Nyerere akisoma wasifu wa Marehemu John Nyerere
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere.

4 comments:

Anonymous said...

Poleni wafiwa but I totally disagree na hii tabia iliyozuka ya kupiga picha maiti. Evan in Western countries they do not do that. Heshima za mwisho is reserved to family members only. But in Tz it is for everybody the viewing. Please let us respect waliokufa na wafiwa pia. Hatuhitaji picha. I have lived overseas, no one does what we are doing.

Anonymous said...

Dr slaa hayo manguo mpaka msibani.Its an insult to politicize msiba banaaa

Anonymous said...

Nakubaliana kabisa na Maoni ya mtu wa kwanza. Waliokufa wanastahili wapewe Heshima zao za mwisho. But, siyo kuonyesha Mwili au Picha kwenye Mitandao!! Viewing inapendeza kwa wana Familia zaidi kuliko Umati wa Watu. Inabidi tubadilishe hii tabia.

Anonymous said...

mbona humsemi nape,mkapa na hao wengine wa ccm waliovaa magwanda meusi ya ccm. achene ushabiki wa kisiasa. sasa na wewe unayesema wasipige picha aliyefariki huu ndio utamaduni. eti umekaa majuu sasa inatusaidia nini sisi, wewe kama unataka kuiga ya huko unakoita majuu ni utumwa wako. utamaduni wetu kila mtu anatoa heshima na picha na kideo tunachukua. acha kujifanya eti majuu endelea kukaa majuu tuachie utamaduni wetu.