ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 12, 2015

Wahamiaji wakwama baharini bila chakula




Wahamiaji wa Asia

Kundi la wahamiaji mia tatu kutoka Mynmar, linasema kuwa limekwama baharini bila ya chakula wala maji kwa siku tatu.
Kundi moja lisilokuwa la kiserikali, liitwalo The Arakan Project, linalofanya kazi na kabila dogo la Rohingya, limeiambia BBC kuwa limezungumza moja kwa moja kwa njia ya simu na wahamiaji hao wanaojumuisha wanawake hamsini na watoto themanini na wanne.

Wahamiaji hao wanasema kuwa, wafanyikazi wa boti linalowabeba wanaaminika kuwa raia kutoka Thailand.

Waliliacha boti hilo siku ya jumapili na kutoweka.

Waliko kwa sasa haijulikani lakini inaaminika ndani ya bahari karibu na kisiwa kimoja cha Malaysia kiitwacho Langkawi.

No comments: