ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 6, 2015

WAZAZI WATAKIWA KUWASAIDIA WALIMU KUONGEZA UFAULU

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Usongwe ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna akigawa vyeti na zawadi kwa wahitimu wa Mahafali ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Usongwe ambapo alikuwa mgeni rasmi.
.Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna akivishwa skafu katika Mahafali ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Usongwe ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna akipokea heshima kutoka Skauti(hawapo pichani)
Wahitimu Meristellah Mosha na Janeth Mmasi wakisoma risala kwa mgeni rasmi.
Wahitimu wakisoma risala yao.
Wahitimu wakiwa kwenye maandamano kuelekea ukumbini.
Wahitimu wakiwa katika ukumbi wa mikutano wakifuatilia matukio
Wanafunzi wa kidato cha tano wakiwaimbia wimbo maalum wanaohitimu
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.


SABABU kubwa ya maendeleo mabovu ya wanafunzi mashuleni sambamba na utoro unachangiwa na baadhi ya Wazazi kushindwa kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya watoto wao, imebainishwa.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Usongwe iliyopo katika mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya mkoani hapa, Benedict Mahenge, katika risala yake kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 6 ya kidato cha sita cha shule hiyo.

Mahenge alisema shule hiyo haina ufaulu mzuri kwa wanafunzi wake hali inayotokana na wazazi kuwaachia jukumu la kuwalea wanafunzi walimu pekee wakisahau kuwa suala la malezi ya watoto linategemea pande zote mbili.

Alisema endapo wazazi watashiriki kikamilifu katika malezi ya watoto kwa kufuatilia nyendo zao kama wanahudhuria masomo kikamilifu itasaidia kuongeza ufaulu kwa mwanafunzi pale atakaoona anafuatiliwa kwa ukaribu kila kona.

Alisema kutokana na wazazi kushindwa kuwa karibu na watoto wao hali hiyo imesababisha kati ya wanafunzi 80 waliokuwa wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano 2013, 57 pekee wamefanikiwa kuhitimu kidato cha sita mwaka huu huku 23 hawajulikani walikoishia.

Mkuu huyo wa shule aliongeza kuwa mbali na wazazi kuchangia ufaulu mbovu wa wanafunzi pia shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa walimu wa hesabu, upungufu wa vitabu, majengo muhimu kama bwalo la chakula ambapo wanafunzi hulazimika kulia mabwenini jambo ambalo ni hatari.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa usafiri kama kuna dharula inatokea ya mwanafunzi kuugua ghafla, upungufu wa vifaa vya michezo na viwanja pamoja na upungufu wa mabweni, vyoo na mabafu kwa wanafunzi wanaolala shuleni hapo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi wa Mahafali hayo, Amani Kajuna, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi(UVCCM), Mkoa wa Mbeya, aliwasihi wazazi kuacha kuwategea walimu katika suala la kulea watoto.

Kajuna alisema wazazi wengi wanafikiri kumaliza kulipa ada bila kufuatilia maendeleo ya motto amekuwa ametimiza wajibu wake jambo ambalo sio sahihi kwani kuna baadhi ya watoto ni wadanganyifu hawafiki shule hivyo ni wajibu wa mzazi kufuatilia mwenendo wake.

“Mzazi kumaliza kulipia ada na michango yote sio kuwa umemaliza kazi jaribu kufuatilia kwa ukaribu ile fedha yako uliyoilipia inafanya kazi kama ulivyotegemea, ukifanya hiovyo utakuwa umemsaidia mwalimu na kiwango cha ufaulu kitaongezeka” alisema Kajuna.

Kuhusu changamoto zilizotolewa na Shule hiyo, Kajuna alisema kutokana na wingi wa wanafunzi ulivyo suala la usafiri wa shule linapaswa kupewa kipaumbele cha pekee ili aweze kulitatua hilo.

Alisema itabidi akutane na Mkuu wa Shule ili waangalie uwezekano wa kupata gari litakalosaidia kulahisisha na kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi pindi dharula kama kuugua linapojitokeza.
Na Mbeya yetu

No comments: