Advertisements

Monday, June 22, 2015

BARAZA LA USHAURI LA WATUMIAJI USAFIRI WA ANGA TCAA-CCC WASHIRIKI KIKAMILIFU WIKI YA UTUMISHI WA UMMA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM

Kikosi kazi cha Watumishi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC) wakiwa tayari kutoa huduma kwa wageni mbalimbali watakaotembelea banda hilo katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Athuman Bakari, Aziza Tamim na Debora Mligo.
Watumishi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC)wakitoa huduma kwa wageni mbalimbali waliotembelea banda hilo leo.

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC), Hamza Johari akizungumza jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari waliotembelea banda hilo.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC), Hamza Johari akiwa katika mahojiano na waandishi wa habari wa Magazeti ya serikali(Daily News na Habarileo) waliotembelea banda hilo Dar es Salaam jana.
 Debora Mligo na Aziza Tamim wa TCAA-CCC wakiwasikiliza wageni waliotembelea banda hilo.
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Charles Chacha  akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC) liliopo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto   ni  Katibu Mtendaji wa Baraza Hamza Johari ,waelimishaji na wahamasishaji  wa baraza hilo Debora Mligo na Athuman Bakari.
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Charles Chacha  (mwenye suti)  katikati akiwa katika picha na  ya Pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC)wakati alipotembelea kwenye banda lhilo  kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments: