ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 22, 2015

FUTARI NYUMBANI KWA BALOZI MWINYI NEW YORK


Naibu mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Matifa Mhe. Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha nyumbani kwake mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York Bwn. Hajji Khamis siku ya Jumapili June 21, 2015 siku Balozi Mwnyi alipofutarisha baadhi ya Watanzania waliopata mwaliko toka kwake na baadae Mhe. Mwinyi kuelezea futari ile itaendelea kufanyika nyumbani kwake kwa mwezi huu wa mfungo wa Ramadhan na atazidi kutoa mwaliko kwa Watanzania wa jimboni mwake kujumuika nae kwenye futari hiyo na kama hukupata mwaliko wake Jumapili hii usiwe na wasiwasi mwaliko wako utakuwepo futari inayofuata.

Kulia ni Mke wa Mhe. Naibu Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa akipata picha na mmoja ya wageni wake.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York, Bwn. Hajji Khamis (kulia) akitoa mawaidha baada ya sala ya magharibi kumalizika.

Naibu mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Matifa Mhe. Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akijumuika na wageni wake kwenye futari aliyowaandalia siku ya Jumapili June 21, 2015 nyumbani kwake New York.

Wakina mama nao wakijumuika pamoja kwenye futari hiyo.

Naibu mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Matifa Mhe. Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akiwashukuru Wageni wake walijumuika nae kwenye futari ya jioni nyumbani kwake na kusisitiza kwamba ataendelea na utaratibu huo wa kufuturisha kwa kuwaalika Watanzania tofati tofauti na kama hukuwepo Jumapili hii usiwe na wasiwasi utajumuika na Watanzania wengine futari inayofuata.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi


No comments: