Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa Iran Nchini Tanzania { ICC } Sheikh Ali Bakar akizungumza katika hafla ya kukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndani ya jengo la Karim Jee Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mabalozi wa Nchi za Kiislamu waliohudhuria hafla ya kukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndani ya Ukumbi wa Karim Jee Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Viongozi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Dar es salaam waliopata fursa ya kuhudhuria sherehe za kuukaribishwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Ayatollah Abbas Kaab Nasab wa Baraza Kuu la Kiislamu la Jamuhuri ya Watu wa Iran akitoa nasaha kwa waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria sherehe za kuukaribishwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan Karim Jee Dar es salaam.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Al – Hajj Mussa Salum akijiandaa kumkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuhutubia sherehe za kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Balozi Seif akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wakati wa sherehe za kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani Mjini Dar es salaam katika ukumbi wa Karim Jee.
Balozi Seif akiagana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Al – Hajj Mussa Salum baada ya kumalizika kwa sherehe za kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Balozi Seif akimuaga Mkuu wa Wilaya ya Ilala Nd.Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadiq mara baada ya kukamilika kwa sherehe za kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Jamii inapaswa kuzidisha wema, na ukarimu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan unaokaribia kwa kuwakumbuka maskini, mafakiri, yatima, wajane na wagonjwa ili kutoa fursa kwa waumini wa dini ya Kiisalmu kutekeleza ibada ya funga kwa moyo thabiti.
Hali hii itafanikiwa zaidi iwapo wafanyabiashara wataacha tabia ya kuongeza bei ya bidhaa zao kitu ambacho huwapa shida wafungaji Ramadhan ambao huhitaji bidhaa hizo hasa za vyakula na nguo za watoto.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa sherehe za kuubaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani zilizotayarishwa kwa pamoja kati ya Baraza Kuu la Bakwata Mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Watu wa Iran zilizofanyika katika Ukumbi wa Karim Jee Jijini Dar es salaam.








No comments:
Post a Comment