Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza katika kikao chake cha kwanza na Watumishi wote wa Wizara tangu alipoteuliwa na Rais hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Juni, 2015. Pamoja na mambo mengine Balozi Mulamula aliwahimiza Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje kufanya kazi kwa bidii, kuwa na utii, nidhamu pamoja na unyenyekevu ili kufikia malengo katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Balozi Mulamula (Hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Mambo ya Nje wakimsikiliza Balozi Mulamula

Juu na Chini ni baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika kikao na Balozi Mulamula

Baadhi ya Watumishi wakichangia hoja wakati wa mkutano kati yao na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula ambaye hayupo pichani

 Mkutano ukiendelea
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya nae akizungumza machache mbele ya Watumishi wakati wa mkutano huo
Balozi Mulamula kwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya wakishangilia kwa furaha wakati walipokutana na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Watumishi wa Wizara wakiwashangilia Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakati wa mkutano pamoja nao. Picha na Reginald Philip |
No comments:
Post a Comment